SPIKA wa Bunge mstaafu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa mkoani Dodoma amevunja ukimya baada kueleza kwamba  Wilaya ya Kongwa ndiyo iliyobeba dhamana kubwa kwa nchi za Kusini mwa Afrika wakati nchi hizo zikipigania uhuru lakini cha kushangaza historia inapotoshwa.


Amesema wakati nchi hizo zinapigania uhuru kila jambo lilikuwa likipangwa katika Wilaya ya Kongwa isipokuwa watu kwa mapenzi yao wameamua kupotosha na kuitukuza Mazimbu huku akisisitiza Serikali inachangia kuuwa historia ya Kongwa na kuibeba Mazimbu iliyoko mkoani Morogoro.

Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo ambaye yuko mkoani Dodoma kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho sambamba na kusikiliza kero za wananchi,  Ndugai ametumia nafasi hiyo kuzungumzia upotoshaji wa historia ya Wilaya hiyo.

Akiwa katika Jimbo la Kongwa ambako Chongolo amefika kukagua pia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, Ndugai amesema Kongwa ndio ilikuwa kituo cha wapigania Uhuru ambapo kwa nyakati tofauti marais wa zamani Samora Machel (Msumbiji) na Sam Nujoma wa Namibia walikaa ingawa baadae wanatajwa kuwa walirudi kuwashukuru wananchi

"Wilaya  ya Kongwa ndiyo iliyobeba dhamana kubwa kwa nchi za Kusini mwa Afrika  wakati wa kupigania uhuru wa nchi hizo kwani kila jambo lilipangwa Kongwa lakini  iwatu kwa mapenzi yao wameitukuza Mazimbu, ",  amesema Ndugai

Amefafanua kwamba kabla ya kuelekea Mazimbu, wapigania uhuru waliishi Kongwa, wakafanya mikakati ya uhuru kwa ajili ya  nchi zao na baada ya kuwa wamejiweka  sawa ndipo wakaanza kutafuta njia za kuwaandaa viongozi kwa kuwapa elimu na hapo ndipo wakaamua kwenda kujenga kituo cha mafunzo eneo la Mazimbu.

Ameongeza kuwa kinachoendelea hivi sasa kila wageni wanapokuja nchini wanapelekwa Mazimbu ambako huko  kumetunzwa vizuri siyo sawa kabisa." Kongwa pameacha pamechakaa lakini Mazimbu kumependezeshwa."

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amekiri kuwa ni kweli   Kongwa imesahaulika na nguvu kubwa imepelekwa Mazimbu."Ukweli hali hii hata mimi inanikera,  kwani Kongwa ndio iliyobeba zaidi historia.






Share To:

Post A Comment: