Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kwa kazi nzuri ya kutekeleza ujenzi wa mradi wa maji wa Magadu.
Naibu Waziri Mahundi ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine amekagua mradi wa maji wa Magadu utakaonufaisha wananchi zaidi ya 23,000 wa maeneo ya kata hiyo kwa ufadhili wa serikali wa Tsh. Bilioni 1.7 kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji.
Mhe. Mahundi amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu na chanzo cha maii ili kuufanva mradi huo kuwa endelevu kwa sasa na vizazi vijavyo.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa ametoa pongezi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watendaji wake wa Wizara ya Maji kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Na Mbunge wa jimbo la Morogoro Mini Mhe. Dkt. Abdulaziz Abood (Mb) pamoja na Diwani wa Kata ya Magadu wameipongeza Wizara ya Maji kwa kazi nzuri na kwa watendaji wa MORUWASA kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kutatua changamoto ya maji katika Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA Mhandisi Tamim Katakweba amesema kuwa mbali na ujenzi wa mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho na kutarajiwa kuanza kuhudumia wananchi kuanzia Julai 2023 na ameshukuru kwa fedha zilizotolewa na Serikali kufanikisha upatikanaji wa maji Morogoro kwa zaidi ya asilimia 100.
Katika ziara yake, Mhe.Mahundi pia ametembelea mradi wa kuhifadhi chanzo cha Maji mto Tangeni unaotekelezwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu na kupongeza juhudi za utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Naibu Waziri Mahundi amepongeza na kufurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya Taasisi za Sekta ya Maji mkoa wa Morogoro.
Post A Comment: