Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh.Omary Kipanga amekipongeza kwa dhati kikosi cha timu ya yanga kwa kuweza kuingia fainali na kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika kivumbi cha michuano ya kombe la shirikisho.


Kipanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mafia alisema kwamba licha ya timu ya yanga kutopata fursa ya kuutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu lakini wameweza kupambana kwa hali na mali katika fainali hizo na kufanikiwa kupata bao la ugenini dhidi ya timu ya USM Alger.

"Kimsingi mimi nikiwa kama naibu Waziri pia ni mdau mkubwa wa mambo ya michezo na kiukweli vijana wetu walikuwa wanaipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ya kombe la shirikisho hakika nawapongeza sana wachezaji pamoja na jopo zima la viongozi kwa kupambana vizuri.,"alibainisha Kipanga.

Aidha Naibu waziri huyo alitoa pongezi zake kwa Rais wa awamu ya sita Dkt.kwa kuendelea kuboresha sekta ya michezo ikiwa sambamba na kuwapa motisha zaidi wachezaji wa yanga hadi wameweza kupambana kuanzia mwanzo hadi kufikia katika hatua ya mwisho ya kucheza fainali.

"Yanga wameweza kutuheshimisha Kama Taifa katika michuano hiyo ya shirikisho na ndio maana na Mimi naungana na Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kuwapongeza kwa kazi nzuri ambayo wameifanya katika medani ya mchezo wa soka,"aliongeza Kipanga.

Katika hatua nyingine aliwataka wachezaji wasife moyo kwani hatua anbayo wameifikia ni heshima kubwa kwa Taifa na kwamba wajipange vizuri na kujiandaa katika michuano mingine ya kimataifa katika msimu ujao kwani pia michezo kwa sasa ni fursa za ajira.
Share To:

Post A Comment: