Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema miradi ya maendeleo inayotekelezwa Manispaa ya Shinyanga kupitia ilani ya chama hicho atahakikisha inakamilika ili iweze kuwanufaisha wananchi.

Amesema hayo leo Jumamosi Juni 24,2023 wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mhe. Mabala ameeleza kuwa hivi karibuni kumetokea mabadiliko ya mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga baadhi ya wananchi wamekuwa na hofu kwenye miradi iliyokuwa ikitekelezwa ambapo amewahakikishia kuwa miradi hiyo ipo kwenye ilani ya CCM na kwamba itakamilika kama ilivyokusudiwa.

“Niwatoe mashaka miradi yote iliyokuwa imeanzishwa na ambayo bado inaendelea kuna watu wameanza kupata mashaka kwa kusema hii miradi haitaendelea niwahakikishie miradi yote iliyoanzishwa ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM na msimamizi wa ilani ni mwana CCM nikiwemo mimi mwenyekiti wa Mkoa miradi yote itakamilika”.amesema Mwenyekiti Mabala

Amesema mpango wa CCM katika Mkoa wa Shinyanga ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ambapo amewaomba wananchi kuendelea kukiamini chama hicho ili kuendeleza msukumo wa maendeleo kupitia viongozi mbalimbali wa serikali na chama.

Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema Chama hicho kitaendelea kuzishughulikia kero zinazowakabili wananchi ikiwezo changamoto katika sekta ya afya, elimu pamoja na miundombinu.

Ametumia nafasi hiyo kumpongeza mbunge wa jimbo la Shinyanga ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi, ajira na vijana Mhe. Paschal Patrobas Katambi pamoja na Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko kwa kuendelea kusimamia vizuri mapato kwenye Manispaa hiyo.

Aidha Mhe. Mabala amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu ili kuimarisha uchumi wa Taifa.

  Akizungumza mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imefanya mabadiliko mbalimbali hasa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali ambapo malengo yaliyopo ni kukusanya takriabani bilioni sita (6) na kwamba mpaka sasa mpango huo umekamilika kwa asiliamia mia moja huku fedha zote yatari zimeelekezwa kwenye shughuli za maendeleo.

Amewahakikishia wananchi kuwa mapato ya Manispaa ya Shinyanga yataendelea kuzinufaisha kata zote huku akiwaomba wakazi wa Manispaa hiyo  kuendelea kuwaunga mkono viongozi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwemo hatua mbalimbali za kuboresha miundombinu na masoko kwa lengo la kuongeza uchumi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ibinzamata Mhe. Ezekiel Sabo amewaomba wakazi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana katika shughuli  za maendeleo ambapo amesema ataendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili kupitia wataalam mbalimbali.

Diwani huyo amesema yapo maboresho mbalimbali yanaendelea kufanyika kwenye miundombinu, masoko pamoja na mazingira ambapo amesema atahakikisha miradi yote katika kata hiyo inafikia malengo yaliyokusudiwa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa ameendelea na ziara zake kutembelea kata za Manispaa ya Shinyanga akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali wa serikali kwa lengo la kupokea na kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Juni 24,2023.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023 kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023 uliofanyika kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023 uliofanyika kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.


Diwani wa kata ya Ibinzamata Mhe. Ezekiel Sabo  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023.

Mkutano wa hadhara ulioratibiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Juni 24,2023.







Share To:

Misalaba

Post A Comment: