Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ameupokea Mwenge wa Uhuru eneo la Tingatinga Wilayani Longido Mkoani Arusha ukitokea Mkoani Kilimanjaro ambapo ulikimbizwa mkoani humo kwa siku saba.
Akipokea Mwenge huo wa Uhuru katika eneo la Tingatinga Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema mwaka huu mwenge huo wa uhuru utakimbizwa kilomita 1168.47 na unatembelea miradi 62 yenye thamani ya bilioni 47,290,543,421.83 ambapo sh,bilioni 31,184,729,891.22 zinatoka serikali kuu na sh,bilioni 1,657,992,282 na halmashauri ni sh, bilioni 3,297238,879.52 wahisani ni sh ,bilioni 11,150,582,378 na wananchi
Alisema miradi 16 itawekwa mawe ya msingi yenye thamani ya shilingi milioni 26,941,819,117.51 ,miradi 14 itazinduliwa yenye thamani ya sh,milioni 11,206,373,826.32 ,miradi 8 itafunguliwa na miradi 24 itatembelewa na kukaguliwa.
Alisema mwenge huo utapita katika halmashauri saba na kwakuanzia unaanza rasmi kufungua miradi na uwekaji mawe ya msingi Wilayani Longido.
Mwenge huo umelakiwa na wakuu wa wilaya za Mkoa wa Arusha,wakuu wa idara wananchi mbalimbali wilayani Longido na Tingatinga.
Naye Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amesisitiza ukaguzi makini wa miradi sanjari na kuwepo kwa taarifa za miradi kwa wakati katika maeneo husika.
Post A Comment: