MAMLAKA ya Afya ya Mimea na viuatilifu nchini -TPHPA imesema itafungua ofisi zake katika Bandari ya Mbamba Bay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ili kusaidia kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na nchi jirani ya Malawi na kuhakikisha mazao yanayoingia na kutoka nchi yana ubora unaostahili .
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo prof Joseph Ndunguru alipotembelea Bandari hiyo akiambatana na Maafisa wa Mamlaka hiyo,na kufanya mazungungumzo na Mkuu wa wilaya ya Nyasa.
Prof Ndunguru amesema katika Bandari hiyo zimekuwepo changamoto kadhaa katiaka ukaguzi wa mazao ambapo ilikuwa ikiwalazimu maafisa wa Mamlaka ya Bandari kufanya kazi zote na kwa kuona tatizo hilo Mamalaka ya afya ya Mimea itahakikisha inafunguo ofisi na kuweka watumishi wenyewe weredi ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nyasa Mh Sanga ameishurukuru mamlaka hiyo chini ya uongozi wa Prof Ndunguru kuwa na maono ya kufungua ofisi katika eneo hilo nyeti nchini .
Mh.Sangacmesema kufunguliwa kwa ofisi hiyo katika eneo hilo kutasaidia kuboresha huduma kwa wananchi.
Amesema suala hilo lilikuwa ni jambo muhimu kwani wananchi wamekuwa wakihangaika pasipo ofumbuzi kwani bidha nyingi kama Mahindi ,pumba pamoja na dawa vilikuwa vikipita hapo kutoka au kuingia nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Post A Comment: