Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameridhishwa na miradi 8 ya maendeleo ambayo Mwenge wa Uhuru imepitia katika halmashauri ya Arusha.
Amesema, miradi yote ipo vizuri ni mapungufu madogo madogo ambayo Wilaya itayafanyia kazi ili kuboresha zaidi.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 8 ikiwemo ya Mazingira, afya, Miundombinu, shule na mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi iliyogharimu zaidi cha shilingi .bilioni 8.5 na kati yake miradi 3 iliwekewa jiwe la msingi, miradi 2 ilizinduliwa na miradi 3 ilitembelea.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Arusha zilianza katika Wilaya ya Longido na zinaendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Arusha.
Post A Comment: