Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Serikali mkoani Shinyanga imesema kampeini ya kitaifa ya msaada wa kisheria ni fursa ya kupunguza migogoro mbalimbali ya wananchi hasa wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama.

Akizundua rasmi kimkoa utekelezaji wa Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria iliyopewa jina la Mama Samia Legal Aid (MSLAC) mgeni rasmi, mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema kampeni hiyo ni fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Amesema kupitia kampeni hiyo wananchi watapata fursa ya kujengewa uelewa katika masuala mbalimbali ikiwemo kutambua haki na wajibu wa misingi ya utawala bora.

RC Mhe.Mndeme amesema ili wananchi wa Shinyanga waweze kunufaika na kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria huduma hiyo itatolewa bure hivyo wananchi wanapaswa kutumia fursa hiyo.

Ametoa wito kwa wananchi Mkoani Shinyanga kutumia nafasi hiyo  kupata huduma ya msaada wa kisheria bure kupitia kampeini hiyo ambayo inaanza leo na kwamba lengo la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii

“Kupitia kampeni hii msaada wa kisheria utatolewa bure katika Halmashauri 6 zote za Mkoa wa Shinyanga kuanzia leo Tarehe 11 mwezi wa sita mpaka tarehe 21 mwezi wa sita Mwaka huu 2023 wananchi wote mnaalikwa kushirikia kupata huduma hizi ambazo zitatolewa katika Halmashauri zetu jitokezeni kwa wingi kampeni hii ni bure wote mtahudumiwa kwa usawa usitoe hata shilingi moja”.amesema RC Mndeme

Aidha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameliagiza jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kushughulikia haraka iwezekanavyo kesi zote zinazohusu ukatili wa kijinsia, ambazo zimekaa muda mrefu kusubiri upelelezi.

Amesema kuwa, watuhumiwa wa kesi hizo ikiwemo zinazohusu ndoa, mimba za utotoni na ubakaji wanapaswa kupatikana haraka na kufikishwa Mahakamani ili hatua zaidi ziweze kuchuliwa.

Mhe. Mndeme amebainisha kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameasisi kampeni hiyo ili kuondoa viashiria vyote vya kuminya upatikanaji wa haki, hususani vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambavyo ndiyo changamoto kubwa katika mkoa wa Shinyanga.

RC Mndeme amewataka wakuu wote wa Wilaya zilizopo katika mkoa wa Shinyanga kwenda kusimamia kwa karibu utekelezaji wa kampeni hiyo na kuwashirikisha viongozi wa ngazi zote wakiwemo Wenyeviti wa Vjiji na vitongoji, watendaji wa Kata na Vijiji, Makatibu tarafa na viongozi wa vyama vya siasa pamoja na kuhakikisha kila kata inayohusika na kampeni hiyo inatenga chumba maalum kwa ajili ya wasaidizi wa kisheria .

Akizungumza naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul, amesema Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya haki jinai katika maeneo mbalimbali ya Nchi, ikiwemo kujenga ofisi ya Mwendesha mashtaka katika mkoa wa Shinyanga.

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Mary Makondo amesema kampeni hiyo itawasaidia wananchi waliowengi hasa wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili.

Naye Meneja rasilimali na mawasiliano wa shirika la Legal Services Facilty (LSF)  Bi. Jane Matinde pamoja na mambo mengine amesema kampeni hiyo itakomesha vitendo vya ukatili.

Mwenyekiti wa uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya  Mama Samia  ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija ametaja baadhi ya mapendekezo ambayo yamelenga kufanikisha kampeni hiyo ikiwemo  kutungwa kwa sheria mahususi ya kupinga ukatili, pamoja na kufanyiwa marekebisho kwa sheria zinazowakandamiza wanawake.

Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kuwa na mfumo maalum wa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Tunapendekeza kuwa na madawati ya malalamiko kwenye ofisi za wakuu wa Wilaya na wawepo wasaidizi wa  kisheria  kwa ajili ya kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi, kwa kutambua ukatili wa kijinsia ni kikwazo katika kuwezesha wananchi kufikia haki kwa wakati ni pendekezo letu kuwa serikali ilidhie kutungwa kwa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia Tanzania na marekebisho ya sheria mbalimbali zikiwemo zinazosababisha ukatili wakijinsia hususan ni kwa wanawake katika sheria ya ndoa na miradhi ambazo bado ni changamoto kwa kwenye jamii”.amesema Bwana Shija

Nao wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava  na Mhe. Santiel Kirumba  wamesema watashirikia kikamilifu katika kuhakikisha huduma ya msaada wa kisheria inawafikia wananchi ili kupunguza migogoro ikiwemo ya Ndoa, Ardhi pamoja na ukatili.Bottom of Form

Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid imelenga kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni na wale wasiokuwa na uwezo, ambapo itadumu kwa takribani miaka mitatu kuanzia mwaka huu.

Kampeni hiyo  imezinduliwa leo Juni 11,2023 ambapo huduma hiyo itatolewa bure na kwamba inakwenda na kauli mbio inayosema msaada wa kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo.

Uzinduzi wa Kampeni hiyo kimkoa ambao umefanyika leo katika uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga, umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma za msaada wa kisheria, wawakilishi wa taasisi na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyokuwa ya Kiserikali pamoja na wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Mary Makondo akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Meneja rasilimali na mawasiliano wa shirika la Legal Services Facilty (LSF)  Bi. Jane Matinde akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya  Mama Samia  ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya  Mama Samia  ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba   akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Donald Magesa akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Hafla ya uzinduzi   Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga ikiendelea.










Share To:

Misalaba

Post A Comment: