Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa Mkoani Arusha imesema kuwa inafuatilia taarifa za diwani wa kataya Sekei Jiji la Arusha Gerald Sebastian za kuchukua shilingi milioni 12 bila kuelezea anazitumiaje fedha ambazo ni kwaajili ya Maendeleo ya Kata hiyo (WDC).

Akizungumza nasi ,Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha Zawadi Ngailo amekiri Taasisi hiyo kupokea madai ya fedha hizo na bado uchunguzi unaendelea na utakapokamilika ikidhibitika ni kweli diwani Sebastian alichukua fedha hizo pasipo kufuata taratibu atafikishwa mahakamani.

"Ni kweli taarifa hiyo tunayo ya diwani kuchukua milioni 12 katika fedha za maendeleo ya kata na tunaendelea na uchunguzi ukikamilika kama tukigundua kuna makosa atafikishwa mahakamani lakini kwa sasa bado tunaendelea kufuatilia suala hili "

Awali Mwenyekiti  wa mtaa wa Sanawari kata ya Sekei, Godfrey Mollel alisema  mtendaji ambaye ni marehemu (Simon Sabagu ) alidanganywa na diwani Sebastian kutoa fedha kwenye akaunti ya WDC na walipomuuliza diwani huyo kulikoni fedha hizo zitolewe bila kufuata taratibu aliwajibu kuwa atazirudisha ndani ya wiki mbili au tatu.

"Tulimbana diwani katika kikao cha WDC na alikiri kupokea milioni 12 na baada ya kukiri alisema atazirudisha tangu mwaka jana hadi leo amerudisha milioni 1 pekee"

Mollel alisema katika kikao cha WDC cha dharura diwani Sebastian alipobanwa alitoa milioni 1 bado tunamdai shilingi milioni 11 na alipotoa hiyo milioni 1 tuliamua kama wajumbe wa kikao cha kujadili Maendeleo ya Kata ya Sekei  (WDC) fedha hiyo aliyorudisha iandikwe kwa jina lake kuwa alichukua shilingi milioni 12 na amerejesha milioni 1

Alisema bado wanamdai milioni 11 lakini pia diwani huyo alidai pia kuna mradi watausimamia Wakala wa Barabara za Mjini naVijijni (Tarura) kwa gharama ya milioni 30 lakini wajumbe hao waliikataa mradi huo hadi waujadili katika kikao chao.

Huku Mwenyekiti mtaa wa Mahakama kata ya Sekei Ahmed Chacha alisema fedha hizo zilitolewa Novemba 15 ,mwaka jana na  walipohoji kama wajumbe wa WDC mtendaji wa kata hiyo Simon  ambaye kwasasa ni marehemu alitoa taarifa za benki iliyoonyesha utoaji wa fedha hiyo shilingi milioni 12.

"Tunahoji kwanini fedha itoke benki bila sisi kujua inatoka kwa sababu gani tunashukuru taarifa zote za utoaji fedha hizo tunazo ingawa mtendaji wa kata amefariki ila nyaraka tunazo na diwani amerejesha milioni 1 bado tunamdai milioni 11 ambazo hatujui anaziridisha lini?".

Alisititiza kuwa ingawa mtendaji wa kata amefariki lakini taarifa zote za utolewaji wa fedha hizi tunazo ila tunahoji kwanini diwani Sebastian achukue hela hivi karibuni kata hiyo ilipata mradi mwingine wa utengenezaji mitaro ya maji mtaa wa Laurei lakini wanahofu watawaeleza nini wananchi kuhusu fedha zilizochukuliwa bila kufuata taratibu.

Alisititiza vyombo vya dola kufanyia kazi taarifa hiyo na kuchukua hatua ili fedha hizo ziweze kurudi na wananchi wapate maendeleo katika kata zao na mitaa. 

Hata hivyo tulipompigia simu  diwani Sebastian kumuulizwa tuhuma za ulaji wa shilingi milioni 12 na kurudisha milioni 1 alipokea na kudai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo sababu limefika Takukuru kwa uchunguzi zaidi.


Share To:

Post A Comment: