Na Okuly Julius-Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amewataka wanaohusika na Usimamizi wa Mazingira kuanzia ngazi ya juu mpaka za Chini Kuimarisha Usimamizi.


Shekimweri ameyasema hayo Leo Juni 4,2023 baada ya Zoezi la Usafi wa Mazingira, kuanzia njia panda ya Meriwa kuelekea makutano ya Swasa na Ilazo Jijini Dodoma, ikiwa ni muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Usafi wa Mazingira Duniani iliyoanza Juni 1,2023 na kilele chake kitakuwa Juni 5,2023.


"Kwa tathmini ndogo niliyoifanya hapa kinachoonekana ni kulegalega Kwa Usimamizi ndio maana Bado tunapata changamoto ya uchafu katika Mazingira yetu hasa hizi mifuko na chupa za Plastiki zimezagaa sana ,


Na kuongeza kuwa "Niwaombe wanaohusika na Usimamizi wa Mazingira kuimarisha Usimamizi kwani mkifanya hivyo hakuna yeyote atakayethubutu kuchafua Mazingira Kwa namna yeyote Ile na adhabu ikiwemo Faini zitumike kwa wale ambao watabainika kuwa wamekithiri katika Uchafuzi wa Mazingira,"amesema Shekimweri



Pia ,Shekimweri amewataka Watendaji wa Mitaa na Kata kutumia suala la Usafi wa Mazingira kama Changamoto na Fursa pia ya kupata mapato Kwa kutumia Sheria zilizopo Kwa wale ambao watakiuka Sheria za utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira.


"Watendaji mnaweza kutumia eneo la Mazingira kama Changamoto au Fursa kwani Kuna Sheria ndogo ya Mazingira ambayo imewapa Mamlaka ya kuwapiga Faini kuanzia laki 3 mpaka milioni Moja Kwa wale wanaoharibu Mazingira hivyo tumieni hiyo kama Fursa ya kuongeza mapato,"amesema Shekimweri



Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amevitaka Vikundi vya Usafi pamoja na Makampuni ya Usafi yaliyopewa dhamana ya kufanya Usafi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma kuwa mfano na kuonesha thamani ya fedha wanazopata kwa kutimiza wajibu wao.


"Kuna vikundi na Makampuni ya Usafi ambazo zilikuja kwetu na Mkurugenzi wa jiji akawapa majukumu ya kufanya Usafi kulingana na makubaliano ila sioni wakifanya bado maeneo mengi yanachangamoto hata huko walikokabidhiwa kufanya Usafi bado haparidhishi,"amesema Shekimweri



Pia amezitaka kampuni hizo kuhakikisha Magari wanayotumia kuondolea taka ni mazima sio wanapozoa uchafu Huku nyuma gari nalo linachafua Kwa kutoa harufu Hilo nalo likashuhulikiwe


Ametoa wito Kwa Wananchi wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza katika kilele Cha siku ya maadhimisho ya wiki ya Usafi wa Mazingira Juni 5,2023,itakayofanyika katika Soko la Wazi la Machinga Complex Bahi Road kuanzia saa kumi na mbili asubuhi huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Andrew Komba ametoa wito Kwa Wananchi na wafanyabiashara kuachana kabisa na matumizi ya mifuko ya plastiki na utupaji wa taka ngumu katika mitaro ya maji ya Mvua kwani ni hatari Kwa Mazingira na Afya Kwa ujumla.


"Tukiamua Kwa pamoja kuachana na matumizi ya vifungashio na mifuko ya plastiki pamoja na utupaji wa taka ngumu katika mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua tutayaweka Mazingira yetu katika Usalama na Mazingira yakiwa safi na salama hata Afya zetu zitakuwa salama,"amesema Dkt.Komba


Mkurugenzi huyo amesema kuwa kutokana na madhara yanayosababishwa na Plastiki katika Mazingira, Dunia imeamua kuja na kauli mbiu ambayo imejipambambanua vyema kuwa ni lazima kupiga vita uharibifu wa Mazingira unaosababishwa na matumizi ya bidhaa za palstiki.



Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo Cha Elimu ya Afya Kwa Umma,Idara ya Kinga, kutoka Wizara ya Afya, Dkt.Tumaini Haonga  ametaja madhara yanayoweza kusababishwa na Uchafuzi wa Mazingira kuwa ni pamoja Magonjwa ya Mlipuko na magonjwa yasioyakuwa ya kuambukiza ikiwemo aina mbalimbali ya Saratani.


"Niwatake wananchi wenzangu kudumisha Usafi wa Mazingira kwani ni tunu ya Afya zetu kwani Mazingira yakiwa machafu ni hatari sana Kwa Afya zetu na viumbe vinavyotuzunguka hivyo hili la Usafi wa Mazingira liwe ni desturi yetu kwani ni njia salama ya kuepukana na Magonjwa ya Mlipuko ikiwemo kipindupindu pamoja na magonjwa yasiokuwa ya kuambikiza kama Saratani



Kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Kitaifa itanyika Juni 5,2023 ,Mgeni Rasmi akitarakiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango na yatafanyika Jijini Dodoma eneo la Soko la Machinga.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: