Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mbute juu ya sintofahamu ya uchimbaji wa madini katika mlima Chilalo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwasikiliza wananchi wa Kijiji cha Mbute wakati wa kuondoa hofu kuwa Mlima Chilalo upo wilaya ya Ruangwa


Na Fredy Mgunda, Nachingwea

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amefanikiwa kuondoka sintofahamu kwa wananchi wa Kijiji cha Mbute iliyokuwa imetanda juu ya uchimbaji wa madini ya Graphite  katika mlima Chilalo

Akizungumza wakati alipofanya ziara katika Kijiji hicho baada kusambaa Kwa video ikionyesha malalamiko ya wananchi juu mlima na msitu wa akiba wa Chilalo kuonekana upo katika wilaya ya Ruangwa na sio Nachingwea.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliwaeleza wananchi kuwa Mlima Chilalo upo wilaya ya Nachingwea na kila shughuli inayofanywa kwenye Mlima huo mapato yote yatakuwa ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea.

Moyo aliwatoa hofu hiyo kwa kuwaambia suala la mipaka linashughulikiwa na serikali ya mkoa wa Lindi kwa ofisi ya wilaya ya Nachingwea ilifanya kazi mgogoro huo ila bado upande wa mkoa na kuhaidi hivi karibuni wataalam kutoka TAMISEMI na ofisi mkoa watafika eneo hilo kutatua mgogoro huo.

Kwa upande wake Afisa madini mkazi mkoa wa Lindi Eng Dickson Joram alisema kuwa leseni iliyotelewa katika eneo la Mlima Chilalo ni leseni ya utafiti na sio ya kuchimbwa kwa madini ya Graphite katika eneo hilo.

Eng Joram alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuondoa hofu kuwa eneo hilo limeanza kuchimbwa madini wakati sio kweli.

Nao baadhi ya wananchi walisema kuwa wanampongeza mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo Kwa kuwapeleka wataalam na kutoa ufafanuzi juu ya uchimbaji wa madini ya Graphite katika mlima Chilalo

"Tumepata ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite  Mlima Chilalo ambao umetulea hofu iliyokuwa imetanda Kwa wananchi"walisema
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: