Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda aelekeza miradi ya uboreshaji miundombinu katika shule za Msingi kukamilika kwa Wakati na kwa ubora uliokusudiwa.
Mhe.Kaganda amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya BOOST katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Serikali imetoa milioni 961.5 za uboreshaji miundombinu ya elimu kwenye Shule za Msingi.
Aidha, Mhe. Kaganda amesema Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imejipanga vyema kuendelea kuwaletea wananchi wake maendeleo ambapo imetoa fedha nyingi za maendeleo katika sekta ya elimu,afya, maji nk
Mhe.Kaganda amewataka wataalum wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuwa na ubora uliokusudiwa kwani anmza ya Serikali ni kuwawezesha Watoto wa kitanzania kupata Elimu bora katika mazingira rafiki.
Post A Comment: