NA DENIS CHAMBI, TANGA.

CHUO Kikuu Cha Mzumbe kimeanza kuhamasisha na kuelimisha wananchi wa wilaya ya Mkinga juu ya fursa mbalimbali  watakazonufaika nazo pindi mradi wa ujenzi wa kampas mpya utakapoanza wilayani humo  sambamba na kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza ili kuweza kukabiliana nazo mapema.

Akizungumza mara baada ya kuwasili na timu nzima  uhamasiahaji  na utoaji wa elimu wilayani humo mratibu wa mradi wa kuboresha  miundombinu na mitaala kwaajili ya mageuzi ya kiuchumi  'HEET' Dk.Christina Shitima alisema kuwa wamepanga kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo kaya zinazoongozwa na wanawake, makundi ya wafugaji, wazee maarufu , viongozi wa dini , viongozi wa kisiasa  pamoja na kukusanya maoni kutoka kwao kabla na baada ya mradi huo.
 
 "Tupo hapa kwaajili ya kuhamasisha na kuelimisha  wananchi na maeneo yote yanayozungukwa na mradi lakini pia kuchukuwa maoni yao tukihamasisha matokeo chanya zikiwemo ajira kwaajili ya kupambania hizo fursa lakini pia kama kuna matukio hasi tuweze kuyaongea kwa pamoja na kuyapangia mikakati tuweze kukabiliana nayo kabla mradi haujaanza "

"Baada ya hapa tutakuwa tunawasiliana na wananchi  ili baadaye mkandarasi atakapokuja aweze kufwatilia yale matakwa ya wananchi  na sisi tutakuwa tunamfwatilia mkandarasi ili tuone ni vitu gani wanavyovitaka na sisi tutakuwa tunapeleka mrejesho kwao" alisema Dr. Shitima

Hata hivyo Dr Shitima kwa niaba ya chuo hicho aliishukuru serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia chuo hicho kuendelea kupanua huduma zake za elimu karibu na wananchi  pamoja na kukipatia ardhi kwaajili ya ujenzi wa chuo hicho.

"Tunashukuru sana serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha kupata huu mradi na serikali ya mkoa wa Tanga kwa kutuwezesha kupata hii ardhi kwaajili ya kuwekeza katika kujenga kampasi ya chuo chetu" aliongeza.
 
 Chuo hicho ambacho kilipokea fedha za mkopo kutoka benki kuu ya dunia kupitia wizara ya elimu sayansi na technologia mahususi kwaajili ya kutekeleza mradi wa kuboresha  miundombinu na mitaala kwaajili ya mageuzi ya kiuchumi  yaani  Higher Education For Economic Transformation (HEET-PROJECT) ambapo serikali ya mkoa wa Tanga imekipatia chuo hicho jumla ya hekali  300 kwaajili ya ujenzi wa tawi jipya katika wilaya ya Mkinga.

Akiwakaribisha wilayani Mkinga mkuu wa wilaya hiyo Kanal Malid Surumbu  wakati wakiwa ofisini kwake alisema  kuwa  ujenzi wa chuo hicho utafungua fursa mbalimbali  zikiwemo za kibiashara utalii  na f uwekezaji hatua ambayo itainua uchumi wa wananchi wa wilaya ya Mkinga.

"Ujio wenu chuo cha Mzumbe katika wilaya yetu ni ishara kuwa  wawekezaji  wa aina mbalimbali watakuja na baadaye ikiwemo ujenzi wa hoteli kubwa ,  tuna mpango wa ujenzi wa soko kubwa la samaki , sekta ya utalii zote hizi ni fursa kwetu na hii ni kutokana na uwepo  Mzumbe tunawakaribisha sana na mimi niwahakikishie ushirikiano wa hali na mali na kuwaambia kuwa mpo salama chini ya kamati ya ulinzi na usalama" alisema Kanal Surumbu.

Timu hiyo kutoka chuo Kikuu Cha Mzumbe kilenga kutoa elimu na uhamasishaji katika vijiji vya Gombero, Vunde,Jihirini, Kichangani, Machimboni, Kwangena, Mjesani, Dima, Mnyezani pamoja na  Machimboni vyote vikiwa katika wilaya ya Mkinga.

Mkuu wa wilaya ya Mkinga (mwenye kofia katikati) akiwa pamoja na wawakilishi wa chuo cha Mzumbe mara baada ya kuwasili wilayani humo leo june 26,2023 tayari kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi kubusu ujenzi wa kampas ya chuo hicho.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya  Mkinga Edwin Mwampamba (katikati) akiwa pamoja na wawakilishi wa chuo cha Mzumbe mara baada ya kuwasili wilayani humo leo june 26,2023 tayari kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi kubusu ujenzi wa kampas ya chuo hicho.
 
Mratibu wa mradi wa kuboresha  miundombinu na mitaala kwaajili ya mageuzi ya kiuchumi  'HEET' Dk.Christina Shitima akisaini kitabu cha wageni wakati walipofika katika ofisi za kata ya Gombero wilayani Mkinga leo june 26 2023
, wapili kulia ni Mratibu wa kitengo cha mazingira kutoka chuo cha Mzumbe na wa tatu ni Mratibu  wa miundombinu wa mradi huo Prosper Leonard. 
Mwenyekiti wa kitongozi cha Pangarawe Mbega Kisua Mbega (aliye simama) akizungumza na kuwakaribisha wageni kutoka chuo kikuu cha Mzumbe mara baada ya kuwasili katika kata ya Gombero tayari kwa kuanza kazi ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uje nzi wa Kampas mpya ya chuo hicho wilayani Mkinga.
 
 
 Mratibu wa mradi wa kuboresha  miundombinu na mitaala kwaajili ya mageuzi ya kiuchumi  'HEET' Dk.Christina Shitima akizungumza na waandhishi wa habari kuhusiana na mradi huo wilayani Mkinga
Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanal Maulid Surumbu (katikati mwenye kofia )  akiwakenye picha ya  pamoja na watumishi kutoka chuo cha kikuu cha Mzumbe mara baada ya kuwasili ofisini kwake kujitambulisha.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wialaya ya Mkinga
Edwin Mwampamba wa pili kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe mara baada ya kuwasili ofisini kwake kujitambulisha.
 

 


Share To:

Post A Comment: