Na, Elizabeth Paulo,Dodoma
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Komredi Daniel Chongolo, amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa Mradi wa barabara kwa kiwango cha lami wa njia nne ya mzunguko (Outer Ring Road) nje ya jiji la Dodoma itakayokuwa na urefu wa kilometa 112.
Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Salehe Juma kuhusu ujenzi wa barabara ya mzunguko yenye urefu wa Km. 112 iliyogharimu sh. Bil. 220.
Chongolo amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo awamu ya kwanza itakamilika mwakani na awamu ya pili mwaka 2025.
Mradi huo wa Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko unatajwa kuwa na manufaa makubwa ikiwemo katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Dodoma na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Aidha Faida nyingine za utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dodoma ambapo magari makubwa ambayo yanakwenda nje ya Dodoma hayatapita mjini bali yatapita katika barabara hiyo huku ajira zaidi ya elfu mmoja zikizalishwa kupitia mradi huo.
Ziara ya Komredi Chongolo ya siku 8 mkoani Dodoma, inahitimishwa leo katika mkutano mkubwa unaofanyika kwenye Uwanja wa Mtekelezo Karibu na Msikiti wa Gadaff Mjini Dodoma.
Post A Comment: