NA DENIS CHAMBI,TANGA

 WAKALA wa usajili wa  biashara na leseni  ‘BRELA’ imewataka wafanyabishara  wote wakubwa,  wakati na wadogo waliopo katika maeneo mbalimbali hapa  nchini  kufuata sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kurasimisha  biashara zao ili kuweza kuchangia pato la Taifa  ambapo pia itawasaidia kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha.

Rai hiyo ometolewa na afisa leseni kutoka BRELA Jubilate Muro wakati akizungumza na wanahabari katika maonyesho ya 10 ya biashara na viweanda yanayofanyika mkoani Tanga ambapo amesma kuwa wapo wafanyabishara wengi wanaofanya biashara wakiwa hawajarasimisha jambo ambalo ni kinyume cha sheria zilizopo ili kujenga uaminifu kwa wateja na wafanyabishara wengine

"Tunawaomba sana wafanyabishara wote nchini wasajili biashara zao kwasababu kuna faida kubwa kwa kufanya hivyo kuliko kutokusajili a lakini pia kuna huduma zingine mfanyabishara ,mmiliki wa kiwanda au kampuni atashindwa kuzipata kwa kukwepa kusajili biashara yake kupitia BRELA"

 “Lakini hii pia itamsaidia kujenga uaminifu kwa wateja wake na wafanyabishara wengine na hata kwenye  taasisi za kifedha ataweza kuhudumiwa kama atahitaji mkopo akiwa na leseni ya kibiahara vinginevyo anaweza kukosa huduma muhimu ambazo zinaweza kumleta maendeleo” 
alisema Muro.

Maonyesho ya biashara na utalii  ambayo hufanyika kila mwaka jijini Tanga yakihusisha makampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali mwaka huu  yakiwa ni ya 10 yamebebwa na kauli mbiu ya ‘Kilimo , viwanda utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’

Kwa upande wake  afisa usajili kutoka BRELA  Julieth Kihwelu alisema kuwa mifumo hiyo ni mikuu pendwa ambayo mwombaji anatakiwa kutumia kuwasilisha ombi lake huku akieleza wanatoa huduma ya kuwafundisha namna ya kutumia mfumo huo kuweza kujisajili.

“Katika mifumo hii mwombaji anatakiwa awe na kitambulisho na Taifa,barua pepe aweze kujisaijili na nitoe wito kwa wajasiriamali nchini kuendelea kusajili alama za biashara zao kwa kuwa alama moja inamtumbisla mtu mmoja”Alisema

Hata hivyo aliwashauri wakazi wa Tanga na mikoa ya jirani waenda kupata huduma ya papo kwa papo ambapo kwa sasa wanaendelea kutoa huduma hiyo katika maeneo hayo.

“Tokea 28 mei mpaka Mei 31 tumekwisha kuwahudumia wananchi 35 na tukilinganisha mwaka jana na mwaka huu kuna utofauti na tunategemea kufikia watu wengi kwa kuwatembele kwenye mabanda hususani wajasiriamali kuweza kuwapa ushauri namna ya kuweza kusajili alama za biashara “Alisema Afisa huyo.
Afisa leseni kutoka wakala wa usajili wa  biashara na leseni  ‘BRELA’ Jubilae Muro akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho  ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya mwahako mkoani Tanga.
Wafanyakazi kutoka wakala wa usajili wa  biashara na leseni  ‘BRELA’ wakitoa huduma na elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya 10 ya biashara na utalii  yanayoendelea katika viwanja vya mwahako Mkoani Tanga.
 


Share To:

Post A Comment: