NA DENIS CHAMBI, TANGA.
MFANYABIASHARA maarufu jijini Tanga aliyefahamika kwa jina Hamis Rashid
(53) mapema leo june 27,2023 amekutwa amefariki katika chumba chake cha
kuhifadhiwa vitu ' Stoo' baada ya kujinyonga kwa kutumia waya wa umeme
huku chanzo cha kuchukuwa uamuzi huo kikiwa bado hakijulikani.
Akitoa
taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa
Tanga Henry Mwaibambe alisema walipata taarifa kutoka kwa mke wa
marehem aliyefahamika kwa jina la Mwanaidi Issa na kusema kuwa jeshi
hilo linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo hicho.
"Mtu
mmoja mfanyabiashara maarufu aliyefahamika kwa jina la Hamis Rashid
amekutwa amejinyonga katika chumba chake cha stoo mpaka sasa hatujajua
sababu gani iliyosababisha achukue uamuzi huo, kwenye chumba chake
tumekuta kwamba alijaribu kujinyonga mara tatu kachukua kamba ya kwanza
imekatika , ya pili ikawa imekatika akakata waya wa umeme ndio
amajinyonya nao"
"Tarifa hizi tumezipata kutoka kwa mke wake
anaitwa Mwanaidi Issa hatujajua chanzo cha kujichukulia uamuzi huo ni
nini, lakini uchunguzi unaendelea tutajua mwisho nini kilisababisha
achukue uamuzi huo" alisema Kamanda Mwaibambe.
Katika tukio
lingine Kamanda alisema kuwa mapema leo june 27, 2023 mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Damian Pius mkazi wa Amboni mwenye umri wa
miaka 24 dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda amekutwa ameuwawa kwa
kupigwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana taarifa za
mashuhuda zikieleza kuwa alikuwa amebeba gunia la mkaa ambalo chini
yake kulikuwa na Mirungi.
"Vile vile mapema leo tuna tukio la
mauaji eneo la barabara ya Utofu Chumbageni mtu mmoja aliyetambulika
kwa jina la Damian Pius (24) huyu Ni boda boda amekutwa ameuwawa kwa
kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani lakini eneo la tukio tuliona
Kama kulikuwa na vurugu, taarifa za mashuhuda Ni kwamba huyu mtu
alikuwa na gunia la mkaa na chini yake kukawa na mirungi waliokuwa
wanagombania hiyo mirungi na mwenzake mmoja akampiga na hiyo nondo"
"Kwahiyo
tumemkamata mtu mmoja anaitwa Oscar Steven Haule (26) ambaye naye Ni
bodaboda mwenzake upelelezi zaidi wa tukio hilo unaendelea" aliongeza
Kamanda Mwaibambe.
Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi
kutokujichukulia sheria mkononi badala take kuwafikisha wahalifu kwenye
vyombo vya dola pale wanapoona matukio karibu na makazi yao.
Post A Comment: