Mbunge wa Tanga Mjini na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo ametembelea wagonjwa waliolazwa katika Kituo cha Afya Makorora na kugawa zawadi kwa lengo la kuwafariji wagonjwa hao. 

Mhe. Ummy ameambatana na Viongozi wa CCM Wilaya ya Tanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Meja Mstaafu Hamisi Mkoba. 

Aidha, viongozi hao wameshiriki kufanya usafi katika Kituo hicho ili kuweka mazingira salama kwa kujiepusha na magonjwa yanayoambukiza. 

Shughuli hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea Mkutano wa hadhara wa CCM Wilaya ya Tanga katika viwanja vya Makorora Sokoni leo tarehe 27 Mei 2023.








Share To:

Post A Comment: