Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Shirika lisilo la
kiserikali la Nancy Foundation limetembelea shule ya msingi Kitangili iliyopo
Manispaa ya Shinyanga na kutoa msaada kwa watoto waliokuwa wakiishi na kufanya
kazi mtaani ambao kwa sasa wanaeendelea na masomo yako shuleni hapo.
Limetoa msaada kwa watoto
hao ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mradi wa kupunguza au kumaliza tatizo la
watoto wanaoishi mitaani na kwamba shirika hilo la Nancy Foundation
linashirikiana na serikali katika hatua mbalimbali za kuimarisha usalama wa
watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Akizungumza katika hafla
hiyo Mkurugenzi wa shirika la Nancy Foundation Bwana Ezra Manjerenga amesema wametoa msaada wa
chakula na kusaidia kuwalipia gharama za masomo ya ziada wanafunzi waliokuwa
wakiishi mtaani.
“Leo
tumefika shule ya msingi Kitangili kilichotuleta hapa ni kuendeleza ufuatiliaji
wa wale watoto waliokuwa wakiishi na kufanya kazi mitaani hapa shuleni
tumebaini watoto saba mahitaji yao muhimu waliyoyaomba ikiwemo vifaa vya shule
lakini tunachokiangalia ni kupunguza muda wao wa kukaa mtaani”
“Leo
tumewalipia watoto wote hawa gharama zao za chakula shuleni lakini pia tumewalipia
hela ya muda wao wa ziada (Tuition) pamoja na bima ya afya CHF ambayo tayari
wazazi wao tuliwasaidia na kikubwa katika mradi wetu tunataka moyo wao
warudishe nyumbani na tupunguze changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi
mitaani”amesema Ezra
Aidha Mkurugenzi wa shirika
la Nancy Foundation Bwana Ezra Manjerenga ameikumbusha serikali kuendelea
kushirikiana katika hatua mbalimbali za kuwaendeleza watoto hao.
“Tunawataka
maafisa ustawi wa jamii, maafisa maendeleo ya jamii na polisi dawati la jinsia
na watoto kuhakikisha kwamba wanaendeleza, tayari wanatakwimu za idadi ya
watoto wanaozurula, tayari watoto wanaelimu ya maadili na tayari watoto wapo
shuleni sasa tunataka tuone mikakati ya serikali kuendelea kufuatilia mienendo
ya watoto ili kutengeneza watoto ambao ni washindi kwa kutengeneza historia yao
ya kuwatoa mitaani “.
“Mpaka
sasa tuliofanikiwa kuwarudisha kwenye familia zao wapo watoto 22 na lengo letu
lilikuwa tufikie watoto 30 lakini watoto ambao tuliwakuta mitaani na
wamefanyiwa dodoso kuhusu maisha yao tunajumla ya watoto 38 ambapo wengine
tunaona wanachangamoto za kawaidi tu sisi tunachukua tunaobaini kweli
wanachangamoto kubwa hasa zinazokwamisha masomo yao shuleni” amesema
Bwana Ezra
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu
msaidizi wa shule ya msingi Kitangili Mwalimu Rachel Dembe amelishukuru shirika
la Nancy Foundation kwa kutoa msaada huo na kwamba itasaidia kupunguza
changamoto za watoto hao.
“Kwa
niaba ya uongozi wa shule sisi tunawashukuru sana Nancy Foundation kwa jinsi
ambavyo mmetusaidia kuwahudumia hawa watoto ili waweze kuhudhuria masomo yao bila
kukosa kwa sababu muda mwingine tulikuwa
tunapata wakati mgumu kuwatafuta lakini tunashukuru kwa msaada mliotupa wa
chakula pamoja na kuwalipia hela ya masomo ya ziada tunategemea hili litakuwa
chachu kwa wanafunzi hawa kuhudhuria shuleni na sisi tunaahidi tutajitahidi
kuwasimamia kama ipasanyo”.amesema Mwalimu Rachal
Naye Mtendaji wa kata ya
Kitangili Mayala Ibrahim amelishukuru shirika hilo la Nancy Foundation kwa
kutoa msaada huku akiahidi kuendelea kushirikiana ili kutimiza mpango wa
srikali juu ya elimu bora kwa watoto.
Post A Comment: