MBULU
Wananchi katika kijiji cha Bargish Antsi wametoa pongezi kwa Serikali kwa uamuzi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi itakayo gharimu kiasi cha shilingi 348,500,000/=,ujenzi ambao utahusisha ujenzi wa madarasa 11 ikiwa ni pamoja na madarasa 2 maalumu kwa ajili ya Wanafunzi wa masomo ya awali.
Pongezi hizo zimetolewa hii Leo katika Mkutano wa Hadhara ulihutubiwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, Kwa Lengo la Kuwahabarisha Wananchi na Kuwashirikisha Kikamilifu Katika Hatua zote zinazo Husu Mradi Huo.
Akizungumza katika Mkutano Huo Komred Kheri James amewaeleza Wananchi kuwa Dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kujenga Shule hiyo Mpya ni Kupunguza Msongamano Katika Shule zilizopo sasa, Kuwasogezea Huduma Karibu Wanafunzi wanao toka umbali Mrefu, na kuboresha Miundombinu ili kuwa na Shule Bora yenye Mazingira wezeshi kitaaluma na malezi.Ujenzi wa shule hii mpya ni muendelezo wa mageuzi makubwa yanayo endelea katika sekta ya Elimu Nchini.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mji wa Mbulu Ndugu Mienzi,Amewakikishia Wananchi kuwa mradi huo utaanza kwa wakati,na utakamilika kwa wakati ukizingatia thamani ya fedha na ubora,na ushirikishwaji wa Wananchi ukiwa ni kipau mbele.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu,Wajumbe wa Kamati ya Usalama, Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Bargish, wataalamu, viongozi wa wananchi na wadau wengine wa elimu.
Pamoja na ajenda maalumu ya mkutano huo, Mkuu wa wilaya pia autumia mkutano huo kusikiliza na kutatua kero na changamoto zilizo ibuliwa katika mkutano huo.
Post A Comment: