Chuo cha uhasibu Arusha (IAA)kimewataka wanafunzi mbalimbali wanaosoma katika chuo cha Uhasibu Arusha kukitumia kituo cha kiatamizi kwa ajili ya kuendeleza bunifu zao na kuweza kufikia malengo yao.
Hayo yalisemwa jijini Arusha na Profesa Eliamani Sedoyeka wakati akizungumza katika maonesho ya mafunzo ya ufundi Stadi yanayofanyika katika viwanja vya Stadium jijini Arusha.
Profesa Sedoyeka amesema kuwa,kituo hicho kimeweza kuwasaidia vijana waliohitimu chuoni hapo kwa kuweza kuanzisha biashara zao mbalimbali na kuweza kujiajiri na hata kuajiri wengine.
Amesema kuwa ,kituo hicho kina malengo mbalimbali ya kuwatafutia mitaji,kuboresha uzalishaji,kuwasaidia kupata masoko ya uhakika na hatimaye kufikia kampuni.
Ameongeza kuwa,kitendo cha kuwaandaa vijana wao kinawasaidia wao kuweza kujiajiri na kuajiri wengine huku kampuni zao zikizidi kukua na kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni kuunga mkono lengo la kujenga Tanzania ya viwanda ambapo kituo kimejipanga kukuza zaidi ya biashara 40 kwa wakati mmoja.
Amefafanua kuwa,vijana wenye wazo la biashara wameweza kuwasaidia kuwa wazo la makampuni ambapo kwa mwaka huu wamewawezesha vijana hao kuanzisha makampuni 6 .
Aidha ameongeza kuwa,kwa mwaka huu chuo hicho kimeweza kuanzisha kozi mpya ya bachelor degree ambayo imewezesha kuzalisha wataalamu wa kutosha ,ambapo amewataka vijana waliohitimu kidato cha sita ndio muda wa kuchangamkia fursa hiyo kwa kujifunza kozi mbalimbali chuoni hapo.
"Sisi tumejipanga kwa kutoa kozi za kimkakati ikiwemo ya uanagenzi katika maswala ya bima,na utalii ambapo wanafunzi wetu wamekuwa wakiandaliwa vizuri na kupata muda mzuri wa kujifunza zaidi."amesema Profesa Sedoyeka.
Post A Comment: