Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeendelea kuweka juhudi katika kulinda afya ya mimea kwa kuhakikisha wanaofanya kaguzi katika shena vipando vinavyoingia nchini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo  kwa wakulima na maafisa ugani pamoja na kufanya ukaguzi wa viuatilifu sokoni ili kuliepusha taifa na upungufu wa chakula.



Hayo yalisema na kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Profesa Joseph Ndunguru wakati akiongea na waandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya afya ya mimea Duniani ambapo alisema kuwa afya mimea inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo visumbufu kwa maana ya wadudu na magonjwa pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayofanya kuwepo kwa ukame hali inayopelekea kupungua kwa chakula na kuharibika kwa hewa safi.


“Asilimia 80 ya chakula inatokana na mimea lakini pia asilimia 98 ya oxygen inatokana na mimea na katika kuadhimisha siku hii mwaka huu kauli mbiu yetu ni Afya ya mimea kwaajili ya kupunguza umasikini, njaa na kulinda mazingira ili kukuza uchumi wa nchi zetu, na ili kuweza kufikia malengo haya ni muhimu kutunza afya ya mimea kwa kuwa na uthibiti ulio mahiri utakaoleta tija,” Alisema profesa Ndunguru.


Profesa Ndunguru alieleza kuwa katika kuendelea kuimarisha afya ya mimea,  TPHPA kwa kipindi cha 2022 hadi April 2023 wameweza kukagua shehena za vipando 189 pamoja na kufanya chunguzi za sampuli 103 za shehena za mimea katika maabara na vitalu nyumba  ambapo zote zilikidhi viwango na kuruhusu biashara kufanyika.


Alisema kuwa kwa kipindi hicho  wamepokea maombi ya vibali 762 vya kuingiza vipando  nchini ambapo vibali 756 vilitolewa sawa na asilimia 99.2, ambapo pia alisema wameweza kutoa mafunzo kwa wakulima 3100 na maafisa ugani 900 katika udhibiti wa mdudu kantangaze na wadudu wengine pamoja na magonjwa.


Alifafanua kuwa katika kuthibiti viwavijeshi mamlaka hiyo ilitoa lita elfu 81563 ya viuatilifu na kusambazwa katika halmashauri 57 za mikoa ya Lindi, Pwani, Morogoro, Tanga, Geita, Mwanza, Kilimanjaro na Manyara lakini pia Lita 561 za aina mbili za viuatilifu zilisambazwa katika halmashauri ya wilaya ya Kilosa.


Aliendelea kusema kuwa kwa kipindi hicho pia wameweza kufanya ukaguzi wa mazao, nafaka na mizizi tani milioni 5, 343, 380 mipakani, bandarini na viwanja vya ndege ambapo kutokana na ukaguzi huo jumla ya vyeti  vya usafi 29,033  vilitolewa na kuruhusu biashara ya mazao kuendea kufanyika.



Alieleza kuwa pia wameweza kuokoa hekari  laki 122,190 dhidi ya mlipuko wa uvamizi wa panya, lakini pia walithibiti makundi  milioni 227 ya ndege aina ya Kweleakwelea na kuweza kuokoa  hekari 1056 ambazo zingeharibiwa na ndege hao, ambapo pia ili kuthibiti inzi wa matunda mamlaka hiyo ilitoa lita 585 za viuatilifu na kusambazwa katika wilaya mbalimbali ikiwemo wilaya ya Muweza, Handeni na kwingineko ikiwa ni pamoja kuthibiti Nzige na kuokoa jumla ya hekari laki 195150.


Katika upatikanaji wa viuatilifu bora profesa Ndunguru alisema kuwa wamesajili viuatilifu vipya 409 na kampuni 198 zilisajiwa katika kipindi hicho ambapo pia wametoa vibali 1324 vya kuingiza shehena za viuatilifu na kati yake  lita milioni 5,837,998 ni viuatilifu vya maji na lita milioni 3, 800000 ni viuatilifu vigumu na jumla ya vibali 802 vilitolewa kwa wafanya biashara wa viuatilifu.


“Katika kuhakiki ubora wa viuatilifu TPHPA imefanya uchambuzi wa sampuli 1025 na sampuli 1005 ambazo zilikidhi viwango   sawa na asilimia 98, ambapo pia tulifanya uchunguzi wa kuwepo kwa viuatilifu katika mazao mbalimbali ikiwemo Parachichi na sampuli 40  zilichunguzwa na kukidhi viwango na kupeleka kuruhusu biashara ya kwenda nje baada ya kuona hazina matatizo,” Alisema.


“Pia tumefanya ukaguzi wa viuatilifu sokoni kwa mikoa 18 na wilaya 72, Machi na Aprili mwaka huu  ambapo tulikagua maduka 1016 na matokeo ya kaguzi hizo yalionyesha maduka 948 sawa na asilimia 93.1 walikuwa wanauza viuatilifu vilivyosajiliwa na kupitisha na mamlaka huku asilimia 6.9 yakionekana kutokuwa na viuatilifu visivyokidhi ubora vingi vikiwa ni vinavyothibiti visumbufu majumbani na asilimia 3 wakipatikana na viuatilifu vilivyotiliwa shaka kutokuwa na ubora na kuondolewa sokoni,” alisema .




Wakulima katika Kijiji Cha Likamba kata ya Musa wilaya ya Arumeru walipotembelewa na mwandishi wa habari hii, mmoja wa wakulima Rehema Obedi alisema mwaka huu wa 2023 wameweza kapanda mimea ikiwemo mahindi, maharage, viazi, shairi, dengu na mboga mboga lakini pamoja na kuwepo kwa mvua zinazoendelea baadhi ya mazao ikiwemo 

Mahindi yamevamiwa na wadudu lakini wamepiga dawa na kwasasa afya ya mimea hiyo inaendelea vizuri.

Share To:

Post A Comment: