John Walter- Kiteto
Mradi huu ufikapo June 30.2023 utakuwa umekamilika kwa
kufungua mawasiliano ya wananchi wa kata za Ndedo na Makame Kiteto ambayo
hayakuwepo.
Meneja wa Tarura Kiteto, mhandisi Edwine Magiri Leo Leo Mei 14.2023 ametaja urefu wa barabara hiyo kuwa ni km 26.8 ambazo
zinatengenezwa kwa fedha za Serikali.
"Fedha hii ni zao la tozo ya sh 100 kwa lita ya mafuta
ambayo inatozwa na Serikali"alisema mhandisi Magiri
"Kutoka Ndedo hadi Makame ni kata mbili tofauti ambapo
kata hizi zilikuwa hazija unganishwa na barabara kwa hiyo barabara hii
tunaifungua ili wananchi hawa waweze kupata huduma muhimu za jamii ambazo awali
hazikupatikana kwenda kwa urahisi maeneo ya Kibaya na barabara kubwa inayoanzia
Ndedo hadi Arusha"
Amesema mradi huu una gharimu sh 514mil ambapo inategemewa
ifikapo June 30.2023 mradi utakuwa umekamilika na kuanza kutumika
"Tunaye hapa mkandarasi kama unavyomuona ameanza kazi
na mashine zake zote ziko saiti, hadi itakapofika mwezi wa sita mwaka huu mradi
utakuwa umekamilika na kuanza kunufaisha wananchi wa kata hizi mbili Ndedo na
Makame ambazo hazikuwa na mawasiliano ya barabara muda mrefu"alisema
mhandisi Magiri.
"Ninachoweza sema hapa mradi huu utakapo tekelezwa na
kukamilika, wananchi wa maeneo haya sasa
watunze miundombinu ya barabara hii kwa sababu awali hawakuwa na
barabara kwa zaidi ya miaka 60 ya Uhuru hivyo barabara hii itaongeza vipato
vyao kama unavyoona hapa tuko kwenye mbuga kuna uhifadhi unaoendelea kwa hiyo
ni kiungo muhimu sana kwa wananchi wa maeneo haya"
Amesema mara nyingi wananchi walilazimika kutumia usafiri wa
pikipiki hivyo huduma ya afya na elimu kwa maeneo haya ilikuwa changamoto
Ally Mgoya Mwananchi kata ya Ndedo alishukuru Serikali kwa
kuona haja ya kujenga miundombinu hiyo ya barabara akisema usafiri wa pikipiki
uliwalazimu kutumia sh 30 elfu kwenda na kurudi na kujikuta wakitumia fedha
nyingi kuliko kufanya maendeleo mengine
"Hili eneo ni mbuga
wakati wa masika halipitiki usafiri pekee ni pikipiki ukitaka kwenda
kata ya Makame kutoka Ndedo lazima utumie sh 30 elfu za kwenda na kurudi ambapo
ni km 26.8" alisema Mngoya
Post A Comment: