Mshauri Mwandamizi katika Usimamizi na Usambazaji wa Dawa kutoka HPSS Bi.Fiona Chilunda,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya kuyajengea uwezo makampuni binafsi yanayotoa huduma ya kusambaza dawa na vifaa tiba yaliyotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kushirikiana na Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) yaliyomalizika leo Mei 3,2023 jijini Dodoma.
Meneja Masoko kutoka Nebula Pharmaceutical Ltd, Linda Barnabas,akielezea umuhimu walioupata katika mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo Makampuni binafsi yanayotoa huduma ya kusambaza dawa na vifaa tiba yaliyotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kushirikiana na Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) yaliyomalizika leo Mei 3,2023 jijini Dodoma.
Idrisa Mziray kutoka kampuni ya Vasco Pharmaceutical Company Ltd ya Jijini Arusha,akizungumzia jisni walivyojifunza kuhusu Teknolojia ya mfumo mshitiri inavofanya kazi ya kuwahudumia wazabuni katika hatua mbalimbali yaliyotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kushirikiana na Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) yaliyomalizika leo Mei 3,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kushirikiana na Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya wamewajengea uwezo makampuni binafsi yanayotoa huduma ya kusambaza dawa na vifaa tiba.
Makampuni hayo ni yale yaliyopata tenda kupitia mfumo mshitiri katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Akizungumza katika mafunzo hayo,jijini Dodoma,Mshauri mwandamizi katika usimamizi na usambazaji wa dawa kutoka HPSS ,Fiona Chilunda amesema kwa siku mbili walikuwa wakiwajengea uwezo makampuni hayo ambayo yanatoa huduma za afya.
Amesema mafunzo yalilenga kuwajengea uwezo wakutumia mfumo ambao TAMISEMI wameutengeneza kwa ajili ya kuagiza na kusambaza bidhaa kwenye vituo vya afya kwa kutumia mfumo mshitiri.
Amesema mfumo huo unatumika nchi nzima.
“Mfumo mshitiri unaruhusu Makampuni binafsi kusambaza bidhaa za afya kwenye vituo vya afya pale tu ambapo Bohari ya Dawa nchini (MSD) watathibitisha kutoweza kusambaza huduma hizo kwenye vituo.”
“Kwa maana hiyo hatutarajii kuwepo na mgogoro wa kimaslahi kwa kuwa mfumo unasaidia upatikanaji wa dawa wakati wote,”amesema Bi. Chilunda.
Kwa upande wake,Idrisa Mziray kutoka kampuni ya Vasco Pharmaceutical Company Ltd ya Jijini Arusha amesema amejifunza jinsi teknolojia ya mfumo mshitiri inavyofanya kazi ya kuwahudumia wazabuni katika hatua mbalimbali.
Amesema teknolojia hiyo ni katika kupokea order na kuhakikisha inafika sehemu husika kwa kufuata utaratibu ambao ni mzuri na m8singi mizuri ambayo imeandaliwa.
“Tunashukuru kwa kutuletea teknolojia hii,tunaamini itasaidia wananchi kupata huduma kwa muda sahihi,”amesema Mziray.
Naye,Meneja Masoko kutoka Nebula Pharmaceutical Ltd, Linda Barnabas, amesema mafunzo hayo yamewasaidia amewapongeza waandaaji wa mafunzo hayo ambayo amesema ni muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za afya.
Amesema mafunzo hayo yatasaidia wananchi kuweza kunufaika na kupata huduma kwa haraka pale ambapo MSD itakwama.
“Wao wataingia katikati na kuwasaidia wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.
“Pia teknolojia itasaidia kuboresha zaidi taarifa za usambazaji wa bidhaa za afya nchini”, amesema Linda.
Post A Comment: