Na; Elizabeth Paulo,Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeweka wazi kukamilika kwa Raisimu ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023.


Serikali imeweka wazi rasimu ya Sera ya Elimu na rasimu ya mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu ambazo zinapatika kwenye tovuti ya wizara hiyo.


Akizungumza leo jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema rasimu hizo zinalenga kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa inaongeza ujuzi ambapo Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 imepitiwa.



"Rasimu za mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu ambayo inakidhi maelekezo ya Rais wetu nayo imekamilika, Serikali imeamua kutoa rasimu hizi ili kupata maoni ya mwisho ambayo tunataka yawe yashapokelewa ifikapo 31 Mei 2023," ameeleza Prof. Mkenda.


Prof. Mkenda amesema Serikali kupiga Wizara imeandaa semina na kongamano mbalimbali ya kuwapitisha wadau katika rasimu hizo ikiwemo semina kwa wabunge wote kuwapitisha kwenye rasimu hizo za mapitio ya sera na Mitaala mipya itakayofanyika may 10, 2023 aidha may 12 - 14, 2023 Kutakua na kongamano kubwa la kitaifa la kujadili rasimu hizo litakalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.


"Serikali imeamua kutoa rasimu hizi hadharani ili kupata maoni ya mwisho Hadi kufikia may 31, 2023, Mwanzoni tulipokea maoni bila kuwa na rasimu tukayachambua na kufanyia kazi, tumeyachakata maoni hayo, tukafanya uchambuzi wa kitaalamu, tumejifunza kutoka nchi mbalimbali na tumetengeneza Rasimu sasa Umma wa Watanzania utaziona Rasimu hizi ili watolee maoni kwenye rasimu hizi ambazo baada ya kuzingatia maoni tutaingiza kwenye michakato ya maamuzi" . Amesema Prof Mkenda




Amesema Wanaotaka kuhudhuria kongamano hilo wanakaribishwa kujisajili ambapo Tangazo la kualika kujisajili linaanza kutoka leo na utaratibu wa kujisajili wa kujisajili utatangazwa lakini Wapo wataalamu na wadau mbalimbali wamepewa mwaliko Rasmi kuja na tutajitahidi kulitangaza kongamano hili ili kila mtu asikilize maoni yanavyotolewa.


 "Watanzania wote popote walipo wanakaribishwa kupitia rasimu hizi na kutoa maoni zao, Rasimu hizi zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo, na Tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania".Amesema Prof. Mwaikenda


Naye katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Mialiko hiyo ipo ndani na nje ya Tanzania ambapo Watanzania wanaoishi nje ya nchi wamealikwa na kutakua na utaratibu maalumu wa kushiriki mjadala huo na kutolea maoni.



"Watanzania wenzetu walioko nje ya nchi watatusaidia kujua kuna nini na watatoa maoni namna ya kuboresha Mitaala hii na sera hii kutokana na uzoefu wao wa nchi nyingine". Amesema Prof. Nombo








Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: