Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi amesema Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura ya 290, kila Halmashauri inatakiwa kuweka utaratibu wa kuwalipa posho, Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji kutoka katika vyanzo vya mapato vya ndani ya Halmashauri.
Ameeleza hayo Bungeni Dodoma wakati alijibu Swali la Mhe.Neema Gelard Mwandabila,Mbunge Viti Maalum, aliyetaka kujua Je, Serikali ina mkakati gani kuanza kutoa Posho kwa Wenyeviti wa Mtaa, Vijiji na Vitongoji ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Ndejembi amesema Spika,Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Kadhalika, amesema Serikali inaendelea kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kubuni na kuimarisha vyanzo vya mapato pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha kwa kutumia mifumo ya kieletroniki ya kukusanya na kutumia fedha katika kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na matumizi mengineyo.
Post A Comment: