NA DENIS CHAMBI.
KAMPUNI ya uuzaji na usambazaji wa mitungi ya gas ORYX mkoani Tanga imefanikiwa kufikisha huduma hiyo kwa wananchi waishio pembezoni na vijijini mkoani tanga hii ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanamfikia kila mmoja sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali katika kupiga vita matumizi ya mkaa na kuni katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupikia.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya kumi ya biashara na viwanda yanayofanyika mkoani Tanga afisa masoko Andrew Noel amesema kuwa licha ya kufanikiwa kufikisha huduma hiyo katika maeneo ya vijijini bado wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya nishati mbadala ili kuhakikisha wanawasaidia kuondokana na adha ambazo zinaweza kujitokeza pindi wanapoendelea kuitumia.
Andrew alisema kuwa kwa kupitia maonyesho ya biaashara yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga ambayo hukusanya makampuni , taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kwa lengo la kutangaza biashara na huduma wanazo zitoa kwa jamii ni fursa ya kipekee kwao kuzidi kuwafikia wateja mbalimbali kwa njia yaelimu wanayoitoa kwa wanaofika katika maonyesho hayo.
“Kama Oryx gas tunajivunia katika huduma zetu na tumeweza kuwadikia wateja wetu mpaka wa vijijini kabisa ambao wapo ndani ndani tuligawa mitungi zaidi ya 600 huu ni mkakati ambao tulijaribu kumsaidia mwanamke ambaye anafanya biashara za ujasiriamali ili kumsaidia katika kuokoa muda wa kufanya baiashara zake”
Aliongeza kuwa Oryx Gas inaendelea kuunga mkono serikali juhudi za kupinga matumizi ya kuni na mkaa kwaaajili ya kupikia ambapo huchangia kwa kiasi kikubwa athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana ukataji wa miti hovyo.
“Tunatoa elimu kwa wateja wetu hasa hasa ya usalama na kuwahimiza wananchi na waeja mbalimbali ambao bado hawajaanza kutumia nishati ya gas waanze kuitumia, mkaa na kuni watu wengi kwa sasa hivi wanaamini kwamba ni nishati ya bei rahisi sana ambayo inawasaidia katika matumizi lakini kiuhalisia nishati ya kuni na gas katika gharama nishati ya gas ni rahisi zaidi kuliko kuni na mkaa” alisema Noel.
“Madhara mbayo yanasab abishwa na kuni na mkaa yako mengi na mengi zaisdi yanaingia katika mfumo wa mapafu na upumuaji kwa kuangalia kwa karibu unaweza ukajihisi uko salama lakini wengi baadaye wanajikuta wana matatizo mbalimbali hii yote inatokana na matumizi ya kuni na mkaa niwasihi sana wananchi tuachane na matumizi ya kuni na mkaa tuhamie kwenye gas mbadala kwa matumizi mbalimbali ili kuodokamna na mabadiliko ya tabaia nchi”
Maonyesho ya biashara ambayo hufanyika kila mwaka jijini Tanga yakihusisha makampuni na taasisi za kise3rikali na zisizo za kiserikali mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya ‘Kilimo , viwanda utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’
katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga Afisa masoko wa kampuni ya kusambaza majiko ya ORYX GAS mkoa wa Tanga Andrew Noel akimhudumia mteja aliyefika katika banda lao kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika mkoani Tanga
Post A Comment: