Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin amekumbusha umuhimu wa kila kiongozi wa chama hicho kushuka chini kwenye mashina ili akutane na wananchi.
Yassin amesema hayo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo ambaye yupo ziarani Mkoani Iringa huku akiwekeza katika vikao vya mashina.
"Tuendelee kukiimarisha chama chetu, Sasa Mimi nitapita huko naamini na viongozi wa maahina yote watakuwa wameshapita," amesema Yassin.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo amesema kwenye mashina ndiko waliko wanachama na sio kwenye ngazi nyingine.
"Huku juu hakuna wanachama, wanachama wapo kwenye mashina huko," amesema Chongolo.
Baadhi ya mabalozi waliozungumzia suala hilo wamedai kuwa viongozi wote wakijenga mfumo wa kuhudhiria vikao vya chini chama hicho litaendelea kushamiri.
Tayari Mkoa wa Iringa uliahafanya mafunzo kwa viongozi wake huku ngazi za Wilaya wakishuka chini kufundisha wajibu wa viongozi wa maahina, matawi na kata.
Post A Comment: