Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb) ametoa Vifaa vya Michezo kwa timu za mpira wa miguu sita katika Kata ya Dabalo kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya Mbunge wa Chamwino.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa viongozi wa timu hizo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki kwa niaba ya Mbunge wakati alipofanya ziara katika Kata ya Dabalo wilayani Chamwino.
Ndejembi ameeleza kuwa vijana wa kata ya Dabalo wamekuwa wakiomba ifanyige ligi ya mpira katika kata kuanzia ngazi ya vijiji vinavyotokana na kata hiyo.
“Kuanzia ligi ya kata inakuwa ni ligi ya Mbunge na ndio maana nimetoa vifaa kama jezi na mipira kuhakikisha ligi inaendelea na Zawadi nitakuja kutoa mimi mwenyewe kwa washindi” amesema Ndejembi
Timu zilizokabidhiwa vifaa hivyo ambavyo ni jezi la mpira ni pamoja na Timu ya Bodaboda, Timu ya Mnadani, Timu ya Chiwondo, Timu ya Igamba, Timu ya Nayu na Timu ya Manyemba.
Post A Comment: