NA DENIS CHAMBI, TANGA.
Taasisi ya mfuko Self Microfinance inayojihusisha na ukopeshaji wa fedha imefanikiwa kuyagusa makundi mbalimbali na shughuli wanazozifanya wananchi hii ikiwa na lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi pale ambapo taasisi na mtu binafsi atahitaji kujiendeleza ili kupata faida zaidi.
Akizungumza na waandishi
wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila
mwaka mkoani Tanga afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance Julius Mungengele
alisema ni lengo la taasisi hiyo kumfikia kila mteja kulingana na
shughuli anayoifanya, taasisi na watu binafsi wenye vigezo ya kuweza
kupata mikopo hiyo yenye riba nafuu pale ambapo watajiridhisha mteja
wao anakidhi kupata mikopo wanayotoa.
"
Lengo kuu la kutoa mkopo kwa mtu hasa ni kumsaidia na sisi tunataka aonyeshe
nia kweli ya kutaka kubadilika na sisi riba yetu ni nafuu na rafiki kwa kila mteja cha kusistiza tu ni kwamba lazima mteja azingatie vigezo na masharti ikiwemo muda wa
mkopo wake"
Mungengele
alizitaja huduma ambazo wanatoa kwa wateja wao ambazo ni pamoja na
mikopo ya kilimo , mkopo wa mkulima, biashara , Imarika, amtaji, mkopo
wa mshahara ambazo wanazitoa kwa riba nafuu kwa wanufaika wao.
"Miongoni
mwa huduma ambazo Self Microfinance finance tunazitoa na zimewanufaisha
wateja wetu na zimegusa zaidi jamii ya watu wa hali ya chini ni mkopo
wa mkulima, mkopo wa kilimo na mtaji lakini pia tunatoa mikopo hii kwa
riba nafuu hasa ya mshabara, biashara na mkopo wa Imarika" alisema
Mungengele.
Aidha
aliwataka wananchi hususani wenye sifa za mikopo zikiwemo wadhamini,
mali inayodhaminika ,leseni za biashara na vitambulisho
vinavyomtambulisha mnufaika kufika katika mabanda hasa kipindi hiki cha maonyesho ya baishara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya
Mwahako ili kupata elimu zaidi.
Pamoja
na hayo alisema mfuko Self Microfinance unaendelea kutoa elimu kwa
wananchi katika kujiendeleza kiuchumi kupitia sekta ya kilimo biashara
huku akiwataka kuchangamkia fursa zinazopatikana ili kuweza
kujiletea maendeleo.
Maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika mkoani Tanga ambayo ni ya 10 mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo ‘Kilimo , viwanda utalii na madini ndio msingi wa maendeleo
ya kiuchumi’
Afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance mkoa wa Tanga Julius Mungengele akitoa elimu kwa Abdul Faraji ambaye ni mmoja wa wateja waliofika katika banda lao kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja v ya Mwahako.
Afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance mkoa wa Tanga Julius Mungengele akitoa elimu kwa wanafunzi wa shulke za msingi waliotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako.
Afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance mkoa wa Tanga Julius Mungengele akitoa elimu kwa wanafunzi wa shulke za msingi waliotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako.
Post A Comment: