Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu, akiongoza kikao cha kawaida cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2020/ 2023 cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoketi May 11, 2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida imeazimia kuliandikia barua Shirika la Taifa
la Maendeleo (NDC) na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) ili kama
yameshindwa kuendeleza eneo la hekta 500 walilochukua kwa miaka zaidi ya 10 kwa
ajili ya uwekeza mradi wa umeme wa jua walirudishe kwa manispaa.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, alisema hayo kwenye
kikao cha kawaida cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2020/ 2023 cha Baraza
la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoketi May 11, 2023.
“Kwakuwa manispaa ndio ilitoe eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji huo kwa hiyo
tutawaandikia barua hayo mashirika ili kama wameshindwa kuwekeza waturudishie
tutafute mwekezaji mwingine,” alisema.
Hatua ya Mkurugenzi kueleza hayo ilifuatia baada ya Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama kuiomba manispaa hiyo kuwasiliana na Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC) ili liweze kurudisha eneo la hekta 500 walilolichukua kwa ajili ya kuwekeza mradi wa umeme wa jua ambalo kwa zaidi ya miaka 10 eneo hilo halijafanyiwa uwekezaji wowote.
"Mheshimiwa Meya eneo hilo ni la wananchi ambao walilitoa kwa ajili ya
kupisha uwekezaji ambao ungefanywa kwa ubia kati ya NDC na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) tangu mwaka 2012 lakini hadi leo hii hakuna uwekezaji wowote
uliofanyika"alisema Mdama.
Mdama alisema eneo hilo lipo Kata ya Unyianga B na lilitengwa kwa ajili ya
uwekezaji lakini kwa kuwa limekuwepo kwa muda mrefu bila kuendelezwa anaomba
lirudishwe kwa wananchi hili waweze kulitumia kwa kilimo na ufugaji.
Aidha, Mdama alisema kama atatokea mwekezaji mwingine apewe eneo hilo kwani
akiwekeza Serikali itapata fedha kutokana na kodi na wananchi watanufaika
kwa kulipwa fidia ambayo hawakupewa wakati likichuliwa na NDC.
Katika hatua nyingine madiwani wa manispaa hiyo wameomba kupatiwa semina
ili waweze kuzijua shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) ambazo wamedai hawazijui vizuri.
Hoja hiyo ilikuja baada ya Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahim Mrua kuzungumzia changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa kata yake waliopo kwenye mfuko huo zikiwemo za kutolipwa fedha zao ambapo aliomba kupatiwa majibu kwenye kikao hicho
"Sisi madiwani tumekuwa na changamoto kubwa ya kujibu maswali ya
wananchi wetu ambao wapo katika mfuko huu wa TASAF hasa pale wanapotuletea
malalamiko ya kutolipwa fedha baada ya kufanya kazi, kuondolewa katika
mpango na ukomo wa umri wa mtu kuwa
ndani ya mpango wa mfuko huo na wale
ambao wanaondolewa," alisema Diwani wa Kata ya Kisaki, Moses Ikaku.
Diwani wa Viti Maalum, Margaret Malecela aliwataka
wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ukimwi kuacha kusubiri vikao vya
baraza hilo ili kutoa taarifa badala yake watoke kwenda kuhamasisha jamii
ichukue tahadhari ya ugonjwa huo jambo litakalo saidia kupunguza maambukizi.
“Hali sio nzuri maambukizi ya VVU kwa wanawake ni makubwa sana kwa kipindi
cha robo ya pili Oktoba hadi Disemba ulifanyika upimaji wa VVU jumla ya wanaume
waliopima walikuwa ni 2,801 na waliokutwa na VVU ni 51 na wanawake waliopima
walikuwa 4,399 waliokuwa na VVU ni 228 huku jumla ya waliopima ni 7,200 na
waliokutwa na VVU ni 279 sawa na asilimia 18,” alisema Malecela.
Meya wa Manispaa hiyo Yagi Kiaratu alisema katika kipindi hicho cha robo ya tatu Januari hadi Machi mapato waliyopata ni asilimia 88 kwa mapato huru na kwa mapato fungwa walirudi nyuma na kufikia asilimia 73 kutokana na watu wachache waliojitokeza kujiunga na mfuko wa bima ya afya wa CHF iliyoboreshwa.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Hassan Mkata akizungumza kwenye kikao hicho
Post A Comment: