Na John Walter-Kiteto
Wilaya ya Kiteto imepokea fedha kiasi cha sh 538,885,960 kutoka Serikalini kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Fedha hizoi zinakwenda kununua dawa na vifaa tiba kama vitanda vya kujifungulia kina mama, vitanda vya upasuaji, mashine za Dawa za usingizi na vipimo mbalimbali.
Fedha hizo ni kwa ajili ya vituo vya Afya vitatu na Zahanati nne ambapo wilaya imepokea jumla ya sh 538,885,960 za miradi hiyo.
Akizungumza hayo kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kiteto Dk. Vicent Gyunda jumapili Mei 14.2023 amekiri kupokea fedha hizo.
Dk. Gyunda ametaja mchanganuo wa fedha hizo kuwa ni kwa ajili ya vifaa tiba na dawa za vituo vya afya na zahanati
"Kituo cha Afya Kijungu Tarafa ya Kijungu kimepatiwa kiasi cha sh 181,711,420, Kituo cha Afya Cha Mwanya Tarafa ya Olboloti kiasi cha Shs 181,711,420"
"Pia serikali imetoa sh 102,982,320 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba Kituo cha Afya cha Engusero kata ya Engusero huku Zahanati ya Ngipa kata ya Engusero nayo ikipatiwa kiasi cha sh 18,120,200"
Alisema kiasi cha sh 18,120,200 kimetolewa kwa ajili ya Zahanati ya Njia Panda Kata ya Namelock huku Zahanati ya Nchinila kata ya Dosidosi nayo ikitengewa kiasi cha sh 18,120,200.
Dk. Gyunda amesema Zahanati ya Magungu kata ya Magungu imepokea sh 18,120,200
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Edward Lekaita kwa niaba ya wananchi wa Kiteto alishukuru Serikali kuendelea kuwapatia fedha nyingi kwaajili ya miradi ya Maendeleo.
"Tunayo kila sababu ya kutoa shukuran kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dk. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendekeo ya wananchi wa Kiteto kwa kweli tumepata miradi mingi.
"Natoa wito kwa watumishi wote kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma za afya kikamilifu na kwa wakati" alisema Mbunge Lekaita.
Post A Comment: