Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe imefanikiwa kuanzisha mradi wa utengenezaji sabuni za aina mbali mbali ikiwa ni moja ya ahadi ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Scolastika Kevela katika kukuza uchumi wa Jumuiya.


Katika zoezi la uzinduzi wa mradi huo ripoti iliyosomwa na katibu wa jumuiya hiyo mkoa Bi.Rehema Mbwana imesema hadi sasa wametumia kiasi cha shilingi milioni 10 kati ya milioni 30 zinazohitajika ili kukamilisha mradi huo.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Njombe Scholastika Kevela amesema kuanza kwa mradi huo ni fursa kubwa katika kuwakomboa wanawake wa UWT.

"Wanawake ni viongozi ndio maana Rais Samia anatuongoza kwa hiyo lazima na sisi tumsaidie kwa kuwajibika kwenye nafasi tulizonazo ndio maana UWT tumeamua kumuunga mkono kwa kuanzisha mradi wa sabuni"Amesema Skolastika Kevela

Akizindua mradi huo mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema mradi huo utasaidia kuondokana na tabia ya Jumuiya za CCM Kuomba omba fedha kwa wadau.

Baadhi ya wanawake wa UWT akiwemo Neema Sigala na Maria Lugome wamekiri kuwa mradi huo umewapa mwanga wa kwenda kubadilika kiuchumi.

Katika hatua za awali mradi huo umeonesha matumaini kwenye jumuiya hiyo kwani tayari wamewapa mafunzo ya utengenezaji wa sabuni hizo baadhi ya wanajumuiya pamoja na vijana.



Share To:

Post A Comment: