Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto wenye ulemavu wa akili na viungo wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity kilichopo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Msaada huo ni pamoja na Mchele, Maharage, unga wa sembe, mafuta ya kupikia, chumvi, juisi, biskuti na Sabuni na kwamba hatua hiyo  ni sehemu ya ziara ya kamati ya utekelezaji Wilaya ya Shinyanga mjini leo Mei 12,2023 kabla ya kutembelea na kukagua uhai wa jumuiya katika kaya ya Kitangili.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana  Fue Mrindoko amesema jumuiya hiyo imeguswa na changamoto zilizopo katika kituo hicho huku akiwaomba wanachama, jumuiya zingine na wadau  mbalimbali kuwa na utamaduni wa kusaidia wetu wenye uhitaji.

 “Jumuiya ya Wazazi tunaendelea kutembelea kata mbalimbali kwa ajili kukagua uhai wa Jumuiya, kuingiza wanachama wapya na kuhamasisha kuanzisha miradi ya kiuchumi na tumekuja hapa kuwatembelea watoto wetu na kuwapatia hiki kidogo tulichokuja nacho na tunaahidi kuendelea kufika hapa na tunaomba wadau wengine na wananchi wajitokeze kusaidia watoto hawa ili kupunguza changamoto”,amesema Mwenyekiti Mrindoko.

“Tunawapongeza sana  walezi wa watoto hawa hii kazi mnayofanya kulea na kuwafundisha watoto hawa mambo mbalimbali kwakweli kazi hii mnayofanya ni kazi ya kubwa mno tunawashukuru na tunawapongeza sana  nimeambiwa watoto hawa walikuwa hawajui chochote lakini mmewafundisha jinsi ya kujitambua na sasa wanafanya wao wenyewe mbarikiwe  sana nasi tunaendelea kukitangaza kituo hiki lakini pia tutaendelea kufika hapa ili tushirikiane kutatua changamoto zilizopo”,amesema Mwenyekiti Bwana Mrindoko

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi ametaja msaada huo kuwa ni pamoja na Mchele, unga wa sembe, Maharage, mafuta ya kupikia, chumvi, juisi, biskuti na Sabuni ambapo amesema jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na kituo hicho katika kupunguza au kumaliza kabisa changamoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother George Paul Rice amesema kituo hicho kina zaidi ya watoto 20 na kwamba ameishukuru jumuiya ya wazazi pamoja na kamati yake ya utekelezaji kwa kutoa msaada huo ambao  utasaidia kupunguza changamoto ya chakula kwa watoto wenye ulemavu wa akili na viungo.

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto wenye ulemavu wa akili na viungo katika kituo cha Brothers of Charity kilichopo mtaa wa Majengo Mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Bwana Fue Mrindoko  akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha Brother of Charity kilichopo mtaa wa Majengo mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Bwana Fue Mrindoko  upande wa kushoto akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha Brother of Charity kilichopo mtaa wa Majengo mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023

  



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother George Paul Rice akizungumza kwenye zoezi la Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini kukabidhi msaada kwenye kituo hicho leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother Francis Bega kizungumza kwenye zoezi la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini kukabidhi msaada leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viongo cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga



Share To:

Misalaba

Post A Comment: