Maji maji maji ni kauli ambayo imekuwa ikitumiwa na Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa katika ziara zake , ndani ya Jimbo Hilo na hii ni kutokana na Jimbo Hilo kuwa na shida /changamoto ya upatikaji wa Maji.
Tarehe 6 May 2023 Mbunge WA Jimbo Hilo Fredrick Lowassa amefanya ziara katika kata ya Selela na Kata ya engaruka Kwa lengo la kuzungumza na wananchi , kusikiliza kero mbalimbali, pamoja na kutoa taarifa za kazi alizozifanya ndani ya uongozi wake na kuahidi utekelezaji wa Haraka .
"Namshukuru mh Rais aliposimama Makuyuni katika ziara yake na kuzungumza na wananchi wa makuyuni ,nilipata nafasi ya kuisemea Monduli na niliomba maji na hakunipa Ahadi kubwa alisema TU nimekusikia mwanangu, niliomba pia Barabara kutoka kigongoni kwenda Engaruka kuelekea loliondo , soko na malisho, namshukuru Mungu wiki iliyopita Document zimefunguliwa kwa maana ya tayari serikali wameshatayarisha fedha za kulipia mradi huo wa billioni 16.4 ,kutoka ngaramtoni kupitia Naalarami, sepeko vijiji 13 vitanufaika na mradi huo Kwa hiyo nimshukuru sana Rais kwani huu ni upendo kwa wanamonduli" amesema Fredrick Lowassa mbunge
"Lakini kuhusu jambo la soko bajeti lilikuwa limepita manake ulikuwa mwezi wa kumi na Moja (11) , Kwa hiyo nilifatilia nikafanikiwa niwaombe wamama zangu wa engaruka naelewa hapa sio mbali , namshukuru Mungu wataalamu walikuja wakaamua Kwa kutuingiza kwenye bajeti ya masoko ya kisasa yanayojengwa na Wizara ya Kilimo mwaka huu wa fedha manake KAZI hiyo itaanza kabla ya terehe 30 mwezi wa 6 ,tumepata soko kubwa linajengwa pale losirwa , naomba sana wanaengaruka hapo sio mbali, mradi ule ni WA fedha nyingi za wananchi walipa Kodi, vijana sanasana hizi KAZI lazima ziwahusu".
"Mimi Kama Mbunge wa wananchi wa Monduli, nawajibika kwenda kuwapa taarifa wananchi walionituma kwa kazi zote ambazo nimefanikiwa kufanya mpaka sasa na kusikiliza mahitaji yao mengine na maelekezo yao Nimewapa taarifa na kuwaskiliza, Na kuahidi utekelezaji wa haraka." Alisema Fredrick lowassa mbunge
Wakizungumza Diwani wa kata ya Engaruka mh Onesmo Naikoyo amesema katika nyanja za Elimu na Afya Adha kubwa waliokunayo imepungua ikiwemo madarasa katika shule ya sekondari ya kata hiyo huku diwani wa selela yeye akiishukuru Halmashauri Kwa kuwapatia shilingi millioni 30 Kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.
Post A Comment: