Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya
shinyanga Mhe. Johari Samizi amewataka wananchi kutoa taarifa za watu
wanaochangia kuhujumu miundombinu katika
miradi mbalimbali ya maendeleo ili serikali iweze kuchukua hatua dhidi
ya watuhumiwa.
Ameyasema hayo leo Mei
10, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mwamalili katika Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga,ikiwa ni ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya
maendeleo
DC Samizi amewahakikishia
wananchi kuwa serikali itaendelea kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika
wilaya hiyo ambapo amekumbusha jukumu la kulinda miundombinu ikiwa ni pamoja na
kutoa taarifa za watu wanaohusika kuharibu miundombinu kwenye miradi ili hatua
ziweze kuchukuliwa.
Aidha Mhe. amizi
amewakumbusha wananchi kuendelea kukemea mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana
na watoto ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za ukatili wanaofanyiwa
wanajamii hasa wanawake na watoto.
“Ukatili
unapotokea tutoe taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa ubakaji, ulawiti vyote
hivyo ni vitendo vya ukatili tusivikumbatie kwa kuona kwamba nikisema mwanangu
amebakwa au mwanangu amelawitiwa eti unaona aibu sisi wazazi tutekeleze
majukumu yetu kwa kuhakikisha kwamba tunawalea na kuwalinda watoto wetu ili
kuepukana na mambo yasiyofaa ambayo yanasababisha mmomonyoko wa maadili hata
maandiko hayajawahi kusema hivyo tunapaswa tukatae ukatili na aina yoyote ya
mmomonyoko wa maadili kwenye maeneo yetu”.amesema DC Samizi
Wakizungumzia suala la
Maadili baadhi ya wananchi wamesema ni jukumu la kila mzazi, mlezi na jamii
kukemea mmomonyoko wa maadili.
Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya
maendeleo ambapo leo ametembelea na kukagua miradi katika kata ya Mwamalili,
Old Shinyanga pamoja na kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Post A Comment: