Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa idara ya makundi maalum SMAUJATA Taifa Bi. Sophia
Kang’ombe leo ametembelea na kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi
wa shule ya sekondari Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Katika ziara ya kutembelea shule hiyo Bi. Sophia Kang’ombe
ameongozana na Bi. Neema Mcharo ambapo pamoja na mambo mengine wametoa elimu ya
ukatili na maadili mema kwa watoto.
Mkuu wa idara ya makundi maalum katika Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii
Tanzania (SMAUJATA) Taifa Bi. Sophia Kang’ombe amewasisitiza
wanafunzi wa shule ya sekondari Town kujiamini na kupaza sauti juu ya ukatili
wanaokutana nao shuleni pamoja na ukatili unaoendelea katika jamii.
Amewasihi wanafunzi hao kutoa taarifa za ukatili sehemu husika
ikiwemo ofisi za serikali za mitaa pamoja na kupiga simu namba ya bure 116 ili
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Aidha mkuu huyo wa idara ya makundi maalum Taifa Bi.
Sophia Kang’ombe na Bi. Neema Mcharo baada ya zoezi la elimu hiyo wametoa
msaada wa vifaa vya shule ikiwemo nguo kwa wanafunzi wenye uhitaji katika shule
ya sekondari Town Manispaa ya Shinyanga.
Bi. Sophia
Kang’ombe amesema zoezi la kutembelea na kutoa elimu katika maeneo mbalimbali
ikiwemo taasisi za elimu ni endelevu hapa Nchini Tanzania.
Mkuu wa idara ya makundi maalum SMAUJATA Taifa Bi. Sophia
Kang’ombe akitoa elimu ya ukatili na maadili kwa wanafunzi katika shule ya
sekondari Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Bi. Neema Mcharo akitoa elimu juu ya ukatili kwa wanafunzi wa
shule ya sekondari Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa idara ya makundi maalum SMAUJATA Taifa Bi. Sophia
Kang’ombe na Bi. Neema Mcharo wakikabidhi msaada wa nguo za shule kwa baadhi ya
wanafunzi katika shule ya sekondari Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga
Post A Comment: