Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi amewataka wananchi hasa wakazi wa kata ya Chibe kutoa taarifa za watu wanaohujumu Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) ili serikali iweze kuchukue hatua kali.

Ameyasema hayo kwenye Bonanza la Michezo lenye kampeni ya ’kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana’’ ambalo limefanyika katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuliwa na viongozi  pamoja na mamia ya wananchi toka maeneo  mbali mbali ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Bonanza hilo limeandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika na taasisi za kifedha ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi.

DC Samizi amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watu watakao kamatwa ama kubainika kuwa wanahujumu rasilimali za serikali.

Amewataka wananchi Wilaya ya Shinyanga kushirikiana na serikali kupitia jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga pamoja na jehi la jadi maarufu Sungusungu kubaini wahalifu hasa wanaohujumu mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaopita katika kata ya Chibe, Old Shinyanga, Isaka pamoja na Luhumbo  na kwamba hali hiyo inakwamisha malengo ya serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi Pamoja na mambo mengine amewakumbusha wazazi na walezi kuwajibika katika suala zima  la malezi na makuzi ya watoto wao ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili.

Amewasisitiza wazazi kulea watoto kwa kuzingatia mila, desturi na tamaduni za Nchi huku akiwaomba wananchi kuwa mabalozi wazuri wa kukataa vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji, ulawiti na ukatili mwingine wa kijinsia unaoendelea katika Wilaya ya Shinyanga.

Amesema wapo baadhi ya wazazi na walezi wenye tabia za kutelekeza watoto ambapo suala hilo hupelekea watoto hao kwenda mtaani kuwa omba omba na wengine kuingia kwenye makundi mabaya ya kihalifu DC Samizi amesema serikali itachukua hatua za kisheria kwa kuwashughulikia wazazi na walezi hao ili kukomesha tabia hizo.

Aidha mgeni rasmi DC Samizi ametumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga pamoja na mratibu Amos John jina maarufu MC Mzungu Mweuzi kwa kuandaa bonanza la michezo ikiwa  lengo ni kuhamasisha jamii kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika Mkoa wa Shinyanga.

Pia ameipongeza timu ya mpira wa miguu ya Radio Faraja FM pamoja na watu wengine waliopata ushindi baada ya kushiriki kwenye bonanza hilo la michezo katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Amewasihi watu wote waliohudhuria bonanza hilo kuendeleza michezo pamoja na mazoezi mbalimbali ya mwili ili kuimarisha Afya zao ambapo amesema hatua hiyo pia itasaidia kuepukana na magonjwa yakuambukiza.

Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna msaidizi wa Polisi  ACP Janeth Magomi ameelezea lengo la kampeni hiyo huku akiwataka  wananchi kutoa taarifa za uvunjifu wa Amani unaojitokeza kwenye maeneo yao.

Kamanda Magomi naye amewaomba wananchi pamoja na viongozi mbalimbali kushirikiana na jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za watu wote ambao hawana mapenzi mema na mradi wa Reli ya kisasa (SGR) unaopita kata ya Chibe, Oldi Shinyanga, Isaka na Luhumbo.

ACP Magomi amewataka wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha kufanya matukio mbalimbali yasiyofaa katika jamii ikiwemo mauaji yanayosababishwa na Imani za kishirikiana, wivu wa mapenzi pamoja na migogoro ya Ardhi.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha watumiaji wa vyombo vya moto wakiwemo waendesha pikipiki hasa wanaobeba abiria (Bodaboda) kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu za usalama Barabarani ikiwemo kutembea na Leseni, kuvaa element na  kutobeba watu zaidi ya mmoja (Mishikaki)

Kamanda Magomi amewahakikishia wananchi pamoja na mgeni rasmi Mhe. Johari Samizi kuwa Mkoa wa Shinyanga ni shwari na kwamba jeshi hilo litaendelea kufanya doria na misako mbalimbali huku akisema wanashirikiana vizuri na viongozi wa Dini (kamati ya Amani) Mkoa wa Shinyanga katika kutokomeza wahalifu.

Baadhi ya wadau waliohudhuria Bonanza hilo akiwemo mwakilishi wa shirika la Haki yangu Foundation Christa Christian wamesema wataendelea kushirikiana na jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga katika juhudi mbalimbali za kupunguza au kumaliza kabisa suala la uhalifu.

Mwakilishi wa shirika la Haki yangu Foundation Christa Christian ameitaka jamii kufikia hatua ya kuondokana na dhana ya kufanya vitendo vya ukatili vinavyohatarisha usalama wa maisha ya Binadamu.

Nao baadhi ya wananchi  wamelipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kufanya bonanza hilo katika kata ya Chibe ambapo wameshukuru kwa elimu na huduma mbalimbali walizozipata kupitia kampeni hiyo ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Awali imefanyika michezo mbalimbali ambapo  washindi wameondoka na zawadi kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu Radio Faraja Fm wameondoka na zawadi ya Mbuzi mmoja, cheti cha kushiriki vyema kampeni hiyo ya kata uhalifu pamoja na Kombe baada ya kuichapa Chibe Combine Fc bao 1-0 ambayo pia timu hiyo imeondoka na zawadi ya mbuzi mmoja.

Mchezo mwingine uliofanyika ni mbio za baiskeli kwa wanawake waliozunguka uwanja wa mpita wa miguu mara 10 mshindi wa kwanza ni Temineta Charles, mshindi wa pili Grace Machiya,mshindi wa tatu Happiness Ramadhani, mshindi wanne Dorcas Amosi na mshindi wa tano Elizabeth Hamis ambapo  Shirika la Haki Yangu Foundation limetoa zawadi kwa washindi wote.

Kwa upande wa mbio za baiskeli kwa wanaume waliozunguka uwanja wa mpira wa miguu mara 50 mshindi wa kwanza ni Kulwa, mshindi wa pili Masele Kichuya, mshindi wa tatu Jelard Kondo, mshindi wa nne Said Kulwa, mshindi tano Wilson Malaika, mshindi wa sita Mahona Kichuya, mshindi wa saba Shune Idasamaga, mshindi wa nane Shija Said, mshindi wa tisa Luhende Mzuzu na mshindi wa 10 Salum Clement na kwamba zawadi  kwa washindi wa mbio za baiskeli zimetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi.

Kampeni ya kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana imefanyika April 15,2023 ambayo imedhaminiwa na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Haki Yangu Foundation, Miti Mirefu Dispensary, Diwani kata ya Chibe, Jeshi la Polisi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi, Soud Bakery, MC Mzungu Mweusi, Kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga ACP Janeth Magomi, Benki ya CRDB, CJ Palace, Tigo, SBC Tanzania Limited, Malicha Microfinance, Juma Nkuba,TARURA, TANROADS, pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Mrisho Satura.

  

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Shinyanga SSP Monica Sehere ambaye ni Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga  akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Picha ya pamoja ya Timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM Shinyanga kabla ya kuanza mchezo

.

Picha ya pamoja ya Timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM Shinyanga kabla ya kuanza mchezo

.

Picha ya pamoja ya Timu ya mpira wa miguu Chibe Combine Fc  kabla ya kuanza mchezo

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikagua timu za mpira wa miguu Chibe Combane FC kabla ya kuanza mchezo.

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikagua timu za mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM kabla ya kuanza mchezo.

Mchezo wa Timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM na Chibe Combine Fc ukiendelea katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Goli ambalo lilifungwa kwa penati na mchezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM Shinyanga.

Mtangazaji kutoka Radio Faraja FM Bwana Elisha Petro akitangaza mechi ya mpira wa miguu ya Radio Faraja wakicheza na Chibe Combine FC

Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani katika Bonanza la Michezo katika uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga kwenye kampeni ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani katika Bonanza la Michezo katika uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga kwenye kampeni ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani katika Bonanza la Michezo katika uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga kwenye kampeni ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Viongozi na wadau mbalimbali wakitazama burudani katika Bonanza la Michezo  uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga katika kampeni ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga BwanaTedson Ngwale akizungumza  kwenye Bonanza la Michezo lenye  Kampeni ya kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria Bonanza la michezo lenye kampeni ya kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana ambalo limefanyika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria Bonanza la michezo lenye kampeni ya kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana ambalo limefanyika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Wadau mbalimbali wakiwa katika Bonanza la michezo kata ya Chibe.










Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi Kombe kwa mwakilishi wa timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM kwa kuwa washindi katika mchezo wao.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: