Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bwana Solomon Nalinga Najulwa,
amewataka wafanyabiashara wote kwenye
eneo lake kuweka walinzi kutoka kampuni zinazotambuliwa na serikali ili kuepuka
udanganyifu
Ameyasema hayo leo April
20,2023 kwenye kikao cha pamoja na
wafanyabiashara wa Mtaa wa Dome kilicholenga kuweka mikakati ya kuzuia mianya
ya wizi,hasa kwenye maduka na maeneo mengine ya Biashara.
Mwenyekiti huyo
amesisitiza wafanyabiashara wa Mtaa huo kuweka walinzi kwa mikataba inayotambuliwa kupitia uongozi wa
serikali ya Mtaa ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.
“Chukueni
kampuni za ulinzi ambazo zinafahamika kisheria na ule mkataba muusome na
muuelewe na kuma mikataba mingine siyo mizuri niwaombe wafanyabiashara kama
kuna watu wanahitaji kuingia mkataba na walinzi ofisi ya serikali ya mtaa ni
mdhamini wa moja kwa moja kwenye mikata hiyo tatizo likitokea kwako wewe
unakuja moja kwa moja ofisini ukitoka hapa tunawasiliana na kata ukitoka kwenye
kata tunawasiliana na mkuu wa kituo ukitoka kwa mkuu wa kituo tunawasiliana na kamanda
wa jeshi la polisi Mkoa”
“Tunahitaji
tuitunze mitaji yetu usihangaike na mtu ambaye hataki kuchangia fedha ya ulinzi
wewe leta taarifa ofisini hapa sisi tutamshughulikia ikiwa ni pamoja na
kutumisha kwenye mtaa wa kwetu bora ikajulikana eneo furani mpo watatu lakini
biashara yetu iko salama kila siku mlizi yupo na mnakuta mali zetu ziko sawa”.amesema
Mwenyekiti wa mtaa Najulwa
Baadhi ya wafanyabiashara
zaidi ya watano (5) wakazi wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya
Shinyanga, wamelalamikia hali ya kukithiri kwa wizi kwenye maduka yao ndani ya wezi mmoja.
Wameeleza kubomolewa
magufuli ya kwenye milango ya biashara yao na kuibiwa vitu na mali mbalimbali
kwenye maeneo yao ya biashara ikiwemo Mchele, Maharage, Simu, Tv, Vocha, gunia
la viazi, Mafuta, Sukari, pamoja na fedha.
Kwa upande wake polisi wa
kata ya Ndembezi Jastin Nyatano amesisitiza suala la wananchi kuchukua hatua za
kuimarisha ulinzi na usalama wa mali zao kwa kushirikiana na jeshi hilo.
Nyatano amewasihi
kuchukua tahadhari juu ya watu wanaoendelea kutapeli kwa kuchukua fedha, mali na
vitu mbalimbalimbali kwa lengo la kulinda mali zao.
Aidha Nyatano amewaomba
wafanyabiashara hao kutoa taarifa za vitendo vya ukatili unaoendelea kufanyika katika
maeneo yao ya biashara kwenye jamii na sehemu zingine ili hatua za kisheria
ziweze kuchukuliwa.
Kikao hicho ulioandaliwa
na Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ulilenga kuimarisha
ulinzi na usalama wa watu na mali zao,ikiwemo maeneo ya Biashara.
Inasadikika wezi hao siyo
wakazi wa mtaa wa Dombe na kwamba baadhi ya wakazi wa Dome kushirikiana na wezi
hao katika hatua za kutambua maeneo ya wafanyabiashara na hadi kufikia hatua ya
kuvunja Magufuli ya milango yao.
Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bwana Solomon Nalinga
Najulwa akiwasisitiza wafanyabiashara wa mtaa huo kuweka walinzi kwenye
biashara zao.
Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bwana Solomon Nalinga
Najulwa akiwasisitiza wafanyabiashara wa mtaa huo kuweka walinzi kwenye
biashara zao.
Kikao kikiendelea katika
eneo la ofisi ya serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
ambacho kimefanyika leo Alhamis April 20,2023.
Kikao kikiendelea katika
eneo la ofisi ya serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
ambacho kimefanyika leo Alhamis April 20,2023.
Kikao kikiendelea katika
eneo la ofisi ya serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
ambacho kimefanyika leo Alhamis April 20,2023.
Post A Comment: