Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi UWT wamefanya ziara ya kutembelea Tarafa ya king'ori iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ili kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakazi wa eneo hilo husani wanawake kukosa mikopo na ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Flora Zelothe na kugundua changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma bora ya Afya
katika Zahanati ya kijiji cha Shishiton iliyopo Kata ya Maruvango kukosa vifaa vya kutolea Huduma na kusababisha wakina mama kujifungulia majumbani.
"Katika sekta ya afya kumekuwa na changamoto kubwa katika Zahanati ya kijiji imekuwa na ukosefu wavifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia wakina mama wajawazito, viti vya kukalia, dawa na vitendea kazi vingine lakini tutajitahidi kulifanyia kazi jambo hili kwa wakati. "
Pamoja na changamoto ya afya vilevile ukosefu wa mikopo kwa wakina mama na vijana limekuwa tatizo kubwa ambapo Mwenyekiti wa UWT Mkoa amewataka wanawake kukuza uchumi wa Taifa kwa kujiunga kwenye vikundi vilivyo sajiliwa ili waweze kupata mikopo inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri.
Suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto limekuwa likikuwa kwa kasi hivi sasa hivyo amewataka wakinamama kuwa makini na watoto kwenye malezi kuwalinda hususani watoto wakiume wamekuwa wakilawitiwa na kuketa madhara makubwa kiafya na kisaikolojia
"Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la ukatili wa kijinsia hususani ulawaiti kwa watoto wa kiume hivi sasa watoto hawana usalama wakienda shuleni wanafanyiwa ulawiti,wakirudi nyumbani pia awana usalama hivyo wakinamama tuwe makini sana katika kuwalinda watoto wetu"
Pia amewataka wananchi wa wilayani Arumeru kuchukua kadi za uanachama ili ziweze kuwasaidia kupata mkopo wa alimia 4 uliyotolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wanawake, vijana pamoja na walemavu.
Wananchi wa Kata ya Maruvango wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana,kutopata mkopo kutokanana kukosa namba ya nida na vikundi vyao kuto kusajiliwa hivyo wameomba serikali iweze kuwasaidia kutatua changamoto hizo,miongoni mwa wahitaji wa kupata mkopo Janeth urio kutoka kijiji cha mbasemi kata ya maruvango
Huku Diwani wa Kata ya Maruvango Majola Godson akamuomba Mwenyekiti wa UWT kuzifanyia kazi changamoto za kata hiyo hususani upatikanaji wa Huduma bora katika Zahanati hiyo.
Post A Comment: