Wananchi wa tarafa ya Mbuguni wilaya ya Meru mkoani Arusha Wametoa kero zao mbalimbali zinazo wakabiri katika maeneo yao wanayoishi ikiwemo maji ya nayo toka katika Mito mbalimbali kujaa mashambani mwao na kusababisha mazao yao kufa.
Kero hizo wamezitoa katika ziara inayoendelea kufanyika na Umoja wa wanawake Tanzania kupia chama cha Mapinduzi UWT wakiongozwa na mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Meru Juliet lameki Maturu huku Mgeni Rasmi akiwa mwenyekiti wa UWT Mkoa Flora Zelothe.
Mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha Mito ili pembezoni na tarafa hiyo kufurika maji yanayokqenda mojakwa moja kwenye mashamba na makazi ya watu imekuwa changamoto kubwa kwa Wakazi wa eneo hilo na hivyo wameiomba serikali iwasaidie kutengeneza muelekeo wa maji
Pia wamekuwa na changamoto ya kukosa maji safi na salama nakupelekea magonjwa ya tumbo kwa watoto na watu wazima vile vile wamehamasisha upandaji miti katika maeneo yao hususani eneo la shule ambapo viongozi wametembelea.
Huku Diwani wa kata ya Majengo Bernad Wilson kivondo akiuomba uongozi wa UWT kulifanyia kazi suala ilo kutokana na kuwa kero kubwa kwa wananchi wake.
" nimejitahidi sana kufuatilia suala hili kwa kina ili kiweza kuondoa maji haya na nilimcuata mpaka muheshimiwa Mbunge ili aweze kutatua hii changamoto alihaifi kuja leo lakini majukumu mengine yamembana hivyo naom a uongozi wa UWT mtusaidie katika hili " amesema Diwani Kivondo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Flora Zelothe amehaidi kuzifsnyia kazi changamoto hizo huku akiwataka wekinamama kupendana na kuto kukatishana tamaa ili waweze kukua kiuchumi na kuwa viongozi bora kuanzia kwenye familia zao.
"Wanawake hatupendani kabisa ukimuona mwenzio anagombea viongozi unaanza kumkatisha Tamara kumsema kuwa ataweza kufuingoza yile na akiwa kiongozi waanza kumsema tumemchagua ameanza kuringa hii inatukisesha kukua hasa katika uchumi"
Pia amewataka wanawake ambao hawajapata mkopo wajiunge na vikundi vilivyosajiliwa ili waweze kupata mkopo huku akisisistiza wale waliopata mkopo na hawajarudisha warudishe mara moja ili wengine waweze kupata.
Ametoa rai kwa madiwani wa tarafa hiyo kuita vikao na kueleza mapato na matumizi yalitotumika katika tarafa hiyo mara kwa mara ili kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu mambo yanayotendeka na serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan
Post A Comment: