Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amemuagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wajasiriamali wapya hawatozwi kodi kabla ya kuanza kufanya biashara.
Mhe. Chande ametoa agizo hilo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, alipotaka kujua ni lini Serikali itaona haja ya kuondoa malipo ya kodi kwa wajasiriamali kabla ya kuanza rasmi kufanya biashara.
Mhe. Chande alisema kuwa Serikali kupitia Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019, Kifungu cha 43 imetoa unafuu wa kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa biashara mpya tangu muhusika anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, lengo likiwa kumpa mjasiriamali nafasi ya kustawi kibiashara.
Post A Comment: