Na.WAF, Dar es Salaam
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana na Kampuni ya SCJohnson ya nchini Marekani katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.
Tukio hilo limehudhuriwa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Mark Martin, Balozi wa Umoja wa Viongozi wa nchi za Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) Mhe. Anthony Okara pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania Mhandisi Leodgar Tenga.
Tamko hilo limefikiwa kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoifanya kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Racine, Winscosin nchini Marekani mwezi Mei, 2022.
Post A Comment: