Viongozi mbalimbali wa Ofisi ya Sheikh Mkoa wa Singida, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) baada ya kupokea msaada wa futari kutoka shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia watu mbalimbali wakiwepo wenye mahitaji maalum.
Dotto Mwaibale na Hamis Hussein - Singida
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO ) Mkoa wa Singida limetoa Sadaka ya Futari kwa Wajane, Yatima, Wazee na watu wengine wenye mahitaji maalum mkoani hapa.
Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida Afisa Usafirishaji wa shirika hilo, Juma Omary alisema shirika hilo limeitikia wito wa Ofisi ya Sheikh wa Mkoa wa Singida ambayo ambaye alitoa wito kwa wadau mbalimbali kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Leo tupo katika tukio muhimu la kuwasaidia wenzetu wenye mahitaji, Sheikh wa Mkoa alitupa ujumbe ili tusaidie jambo hilo kwa kuwa shirika letu linashughulika na kuhudumia jamii tukaona tuitikie wito huo kwa kuwa ni wajibu wetu kurudisha faida kidogo tunayoipata kwa jamii," alisema Omary.
Omary alipongeza Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kuwa kiunganishi na Jamii na kuwa shirika hilo linaunga jitihada za Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Subeiry Bin Ali na Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro za kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwepo Yatima na Wajane.
Afisa Uhusino na Huduma kwa wateja wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo alisema Tanesco imekuwa ikihudumia jamii hivyo inaungana na watu wenye uhitaji katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo alitumia nafasi hiyo kuiomba ofisi ya Sheikh wa mkoa kuliombea shirika hilo ili liendelee kuwahudumia wananchi.
Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro amelishukuru shirika hilo kwa kuwaajali wenye uhitaji ambapo ametumia nafasi hiyo kuyataka mashirika na taasisi zingine kuiga mfano kutoka Tanesco wa kusaidia jamii badala ya kusubiri wadau kutoka nje ya nchi.
Nassoro alisema kuwa wajane na Yatima ni watu wa karibu na jamii kwa historia ya ukoo na dini pamoja na utanzania ambapo aliwataka wadau wengine kuwa na moyo wa huruma wa kusaidia jamii.
“ Nawashukuru sana Tanesco Mkoa wa Singida kwa kuwajali wenye uhitaji na nitowe wito kwa mashirika mengine kama vile viwanda vya mafuta, na taasisi zingine kuiga mfano wa huo kwa kuwasaidia wajane, Watoto yatima, wafungwa wa magereza ni aibu kuona watu kutoka Uturuki na Misri kuwasaidia ndugu zetu” . Alisema Sheikh Nassoro.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kitengo cha Kusaidia jamii yenye Uhitaji kama vile Wajane, Yatima na Wazee ambao hawajiwezi cha Nusrati Al Ummati, Ally Amani aliishukuru Tanesco Mkoa wa Singida kwa kutoa Futari hiyo pamoja na Taasisi ya Sheikh Arfu ambayo imetoa Tende.
“Mashallah wapendwa kaka zetu, Wapendwa shirika letu la Tanesco tunashukuru sana kwa msaada mliotoa kwetu tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi na kuwatimilizia mahitaji yenu karibuni tena kwenye ofisi ya Sheikh wa Mkoa wa Singida.
Aidha, Amani alimshukuru Sheikh Arfu na kampuni yake kwa kuwapelekea tende boksi 20 kwa ajili ya kusaidia makundi hayo.
Picha ya pamoja wakati wa hafla yakupokea msaada huo toka Tanesco.
Afisa Usafirishaji wa shirika hilo, Juma Omary (wa nne kutoka kulia) akizungumza na viongozi wa ofisi ya Sheikh wa Mkoa wa Singida wakati wa kukabidhi msaada huo.
Afisa Usafirishaji wa shirika hilo, Juma Omary (katikati) akimkabidhi msaada huo mmoja wa wahitaji. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro. Zawadi zikiwa zibeshikwa tayari kwa kutolewa kwa wahusika.
Msaada huo ukitolewa kwa wahusika.
Msaada huoukipokelewa.
Wakina mama wakisubiri kupokea msaada huo.
Post A Comment: