Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi
wa jamii Tanzania SMAUJATA idara ya makundi maalum Mkoa wa Shinyanga Bi. Sophia Kang’ombe amewakumbusha
wananchi kutoa taarifa za ukatili unaoendelea kwenye jamii.
Bi. Sophia Kang’ombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa SMAUJATA
Manispaa ya Shinyanga, afisa ustawi wa jamii na msimamizi wa kituo cha makazi
ya wazee na wasiojiweza Kolandoto ameisihi jamii na wadau mbalimbali kuendelea
kuiunga mkono serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili unaoendelea Mkoa
wa Shinyanga.
Amesema serikali inafanya jitihada mbalimbali za
kupambana kutokomeza vitendo vya ukatili hivyo ni muhimu wadau na jamii
kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa ili hatua zaidia za kisheria
zichukuliwe.
Aidha Bi. Sophia Kang’ombe ameyasema hayo kwenye hafla
iliyoratibiwa na watumishi kutoka chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa ajili
ya kutoa msaada katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto Mkoa
wa Shinyanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto Mkoa wa Shinyanga Bwana Kija Nyipuke naye ameiomba jamii kushirikiana na serikali katika kudhibiti ukatili ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi
wa jamii Tanzania SMAUJATA idara ya makundi maalum Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa SMAUJATA
Manispaa ya Shinyanga, Bi. Sophia Kang’ombe akizungumzia suala la jamii kutoa
taarifa za ukatili kupitina namba 116
Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi
wa jamii Tanzania SMAUJATA idara ya makundi maalum Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa SMAUJATA
Manispaa ya Shinyanga, Bi. Sophia Kang’ombe akizungumzia suala la jamii kutoa
taarifa za ukatili kupitina namba 116
Mwenyekiti wa kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza
Kolandoto Mkoa wa Shinyanga Bwana Kija Nyipuke akiiomba jamii kudhibiti vitendo
vya ukatili Mkoa wa Shinyanga
Post A Comment: