Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi amesema serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa Dini katika kuendeleza amani na umoja Nchini.

Ameyasema hayo leo April 22,2023 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na waumini wa Dini ya kiislam kwenye Baraza la Eid El Fitr ambalo limefanyika katika  ukumbi wa Mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani.

Naibu Waziri Mhe. Paschal Patrobas Katambi amesema serikali inatambua umchango unaofanywa na taasisi za Dini ambapo amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hizo ili kuendeleza umoja na amani ya Taifa.

Amewasihi waislam kuendelea kuyaishi yale mema ambayo wamekuwa wakiyafanya katika kipindi cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa ramadhan ikiwemo upendo, majitoleo, kusaidia watu wenye mahitaji pamoja na kuombea Nchi na viongozi wa serikali.

Serikali yenu inawatambua inawaheshimu na inawasikiliza tutaendelea kushirikiana siku zote kwenye mambo ya kiimani na mambo mengine ya muhimu yasiyoya kijamii”.

“Tumemaliza siku zetu hizi 30 lakini tuendelee kuyaishi yale ambayo tumeyaishi katika kipindi chote cha mfungo lakini pili tuendelee kuwa na upendo, kuwa na moyo wa subira, kutoa sadaka, kuwaombea wengine na kuwasaidia watu wenye uhitaji”.amesema Mhe. Katambi

Aidha Mhe. Katambi amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kukemea mmomonyoko wa maadili kwa vijana huku akiwataka wazazi na walezi kufuatilia tabia za watoto wao ili kuwaepusha kuingia kwenye makundi yasiyofaa.

Naibu Waziri Mhe. Katambi amewahakikishia kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kutatua changamoto za wananchi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Katika Baraza hilo mjumbe wa BAKWATA Wilaya ya Shinyanga Bwana Hussen Mohamed Kheri amesema risala ambapo mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi amepokea na kuahidi kutatua changamoto zilizopo ikiwemo changamoto ya usafiri pamoja na vyombo vya matangazo ( Vipaza sauti) ili kuendelea huduma za kiimani.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya amesisitiza upendo kwa watu wote huku akihimiza baadhi ya vyama vya kisiasa Mkoa wa Shinyanga kuacha utengano wa kubagua Dini wala Kabila na kwamba wanapaswa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kidini pamoja na shughuli za kijamii.

“Hapa Shinyanga kuna baadhi ya vyama vina udini kweli kweli na hasa nyakati za uchaguzi ukifika utaona wanachaguana kwa kuangalia udini na yule ambaye atakuwa siyo Dini yake atapigwa chini hili nimelifuatilia na nimeligundua hili linatuvunjia heshima yetu kwahiyo sisi udini hatuutaki katika Mkoa wa Shinyanga lakini pia kuna ukabila upo nao siyo mzuri katika Mkoa wetu”.amesema Sheikh Makusanya

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi akizungumza leo April 22,2023 kwenye Baraza la Eid El Fitr katika  ukumbi wa Mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani.

 Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akizungumza kwenye  Baraza la Eid El Fitr katika  ukumbi wa Mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani.

Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Suleiman Kategile akizungumza kwenye Baraza la Eid El Fitr katika ukumbi wa mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi awali akipokelewa na Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Suleiman Kategile.

Baraza la Eid El Fitr likiendelea katika ukumbi wa mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani leo April 22,2023

Baraza la Eid El Fitr likiendelea katika ukumbi wa mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani leo April 22,2023

Share To:

Misalaba

Post A Comment: