OR-TAMISEMI
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt.Charles Wilson Mahera amesema kufikia mwaka 2023 jumla ya X-ray za kisasa za kidigitali 213 zimesimikwa, Utra sound 67 zimesambazwa na kusimikwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya msingi.
Vifaa tiba vingine vilivyosambazwa ni pamoja na portable X-ray 108 ambazo zitatoa huduma kwenye majengo ya dharura (EMD) yaliyojengwa kwenye halmashauri 80 nchini na majengo 28 ya wagonjwa mahututi (ICU).
Ameyasema hayo leo kwenye kikao kazi cha wadau kujadili rasimu ya mtaala wa astashahada ya radiolojia kilichofanyika jijini Dodoma.
Aidha, Dkt.Mahera amesema, katika mwaka wa fedha 2022/23 Ofisi ya Rais TAMISEMI ilifanya upembuzi yakinifu na kujiridhisha kuwa kufikia mwaka 2032 jumla ya wataalamu 13,178 wanahitajika kutoa huduma za radiolojia katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Dkt.Mahera amesema, "endapo mtatumia fursa hii vizuri ni lazima tutapata mtaala bora ambao utatuwezesha kupata wataalamu wa radiolojia, wataalamu ambao watakwenda kufanya kazi na kutoa huduma bora za uchunguzi katika mamlaka za serikali za mitaa."
Post A Comment: