Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe, John Mongela amewataka viongozi wa ngazi zote kuanzia Dc,Meya,Mkurugenzi pamoja na madiwani kufanya kazi zao ipasavyo kama walivyo aminiwa na kupewa nafasi hizo na kuacha kusikiliza maneno ya mitaani ambayo hayana maslahi kwa wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla.
Mongela ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa wiki ya muungano ambapo amefungua vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari kaloleni vilivyojengwa na halmashauri ya jiji la Arusha kupita fedha za hazina ambapo kwa jiji la arusha ilipata shilingi milioni 980 ambazo zimejenga shule mpya mbili, vyumba vya madarasa 9 pamoja na vyoo, Pamoja na fedha za mradi wa BOST ambapo arusha imepata shilingi milioni 940.9 ambazo nazo zimejenga shule mpya mbili pamoja na vyumba vya madarasa 13.
Rc Mongela amesema kwamba kwasasa kumekuwa na maneno ambayo hayana faida kwa wananchi wa jiji la Arusha hasa pale watu wanapo taka kutengenezea ajali ambazo hazina faida yeyote katika maendeleo kwa wananchi.
"Niwaombe Dc, Meya, Mkurugenzi, pigeni kazi maana nyie mnayo maelekezo na mimi ndiyo ninao wasimamia na sio mwingine msitoke barabarani za maneno ya watu wa barabarani maana kuna mbinu nyingi za kuondoana kwenye muelekeo". Amesema Mongela.
"Madiwani shirikianeni na muweze kulishika Jiji lenu msikubali upuuzi na kuburuzwa, maana huku mtaani mnaheshimika, mnafika kwenye baraza mnajifanya hamnazo, Wana Arusha ni waelewa na wanaweza kuchambua pumba ni zipi na mchele safi ni upi, Arusha hatutekenyeki kirahisi". Ameongeza Mongela.
"Hapa jiji palitokea ubadhilifu na kesi zinaendelea tuache sheria ichukue mkondo wake leo hii anatokea mtu anabwabwaja kama hana malezi, imetokea hii ukiwa kiongozi na wewe mwenyewe ndiyo unakuwa wakwanza kupiga mayowe yasiyo kuwa na maana kama umehishiwa hoja omba ushauliwe na wenye hekima". Aliongeza mongela.
Pia Rc Mongela ameeleza kwamba Arusha ni Mkoa ambao uko salama pamoja na maendeleo yake endelevu na hakuna siku changamoto zikaisha ma kwamba kwa watu wenye uwelewa huwa hawapayuki hadharani katika kutatua changamoto ni vyema wote msemezane na muwe na muweze kupata maadhimio ya pamoja.
"Yani unajiibia alafu unapiga mayowe mwenyewe ili kusaidiwa na unapo ulizwa mwizi nani unasema nilisikia, kumbe wewe mwenyewe ndiyo mwizi ila hujinyooshei kidole wewe ila unanyooshea wengine". Amesema Mongela.
"Ukiona mtu anawanyooshea vidole wenzake vikojozi basi ujue yeye ndiyo kikojozi mkubwa, ukiniona nimelipuka ujue wananchi wamekosewa sana ma sipo tayari kuona wananchi wanakosewa maana kila jambo lipo ndani ya ilani yetu ya chama, Ukiona mke na mume wanapigana hadharani hapo ndani changamoto ni kubwa sana, mnatakiwa kuwa wasili panapo tatizo na wageni wakiondoka ndiyo muendelee kuraruana". Alionheza mongela.
Aidha katika suala la wafanyabishara Mhe, Mongela amesema kwamba Jiji la Arusha halina hati miliki ya mtu mmoja wala kikundi cha watu na ameweza kuwaelekeza kamati zake ziweke kuweka miundombinu sahihi kwa wafanyabiashara wa aina yote na kwamaeneo husika.
"Katika Jiji hili hakuna miliki ya mtu sasa tutapanga makundi yote ya wafanya biashara, bodaboda pamoja na machinga kwa mipango mizuri na kufanya biashara zao ziwe na manufaa zaidi". Amesema Mongela.
"Mstahiki meya fanyeni kazi msifuate mambo ya watu watumikieni wananchi wenu waliyo waamini maana nafasi hizo mlizo nazo nizakuwatatulia wananchi changamoto zao, tutatutie changamoto nasiyo kuzikimbia maana wote mkianza kulia haifai na wote tuwe wamoja wala haifai kushikiana akili wala kufuata ya mtu mmoja huo ni udhaifu mkubwa". Aliongeza Mongela.
Aidha katika hatua nyingine Rc Mongela amewataka viongozi mbali mbali mbali kukemea kwa pamoja na kupiga vita swala la mapenzi ya jinsia moja pamoja na ushoga na kueleza kwamba anazo taarifa mbali mbali za taasisi hapa arusha kufanya matendo hayo na kutoa onyo kali kwa watakao bainika.
"Kwa arusha zinatajwa taasisi kadhaa zinazo shughulika na haya mambo nimeshatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili tuwabaini tushughulike nao. Nataka niwambie tusipo kuwa makini hata viongozi kwa miaka 50 mingine ijayo watakuwa wanang'ata kucha maana hili ni tatizo linatengezwa tusipo lipinga haraka tutajikuta tumezama". Amesema Mongela.
"Katika Mkoa wa Arusha akatokea mtu akashabikia ushoga na akitaka kuendekeza mambo ya ushoga, mapenzi ya jinsia moja na ulawiti hatutovumilia tutamshughulikia ipasavyo, kama wewe unataka ushoga jifungie ndani kwako ufanye mambo yako mwenyewe na ukitaka kufanya haya mambo fanya mwenyewe usiwe sehem ya kuharibu jamii". Amesema Mongela.
Aidha Mongela ameweza kuwahasa vijana ambao ni wanafunzi mbali mbali kwa kuwataka waweze kusoma kwa bidii maana vijana ndiyo tegeo la kesho katika mataifa yote ya Afrika na ndiyo maana serikali inapambana kumuwezesha kijana kupata elimu bora na stahiki.
"Mhe Rais anaendelea kupambana katika kuikuza elimu hapa nchini niwasihi vijana zingatieni elimu itawaokoa maana kwasasa dunia inaelekea kubaya hasa katika wimbi la mapenzi ya jinsia moja na watoto wakiume mkiona walimu wanaanza kuwapapasa au kijana mwenzio kataa na toa taarifa mapema tuweze kuangaika nao". Amesema Mongela.
"Niwaombe viongozi wengine tusaidiane kufuatilia na taarifa zipo watu wamepanga majumba makubwa wameweka mageti makubwa humo ndani wanafanya ushenzi nimesema nitawafuta popote ili tuweze kuwavhukulia hatua kali za kisheria". Alisema Mongela.
Awali Akitoa ufafanuzi wa ujenzi huo wa madarasa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Hergney Chitukulo amesema Jiji la Arusha lilipokea fedha za BOST shilingi Milioni 940.9 pamoja na fedha za Hazina kiasi cha shilingi milioni 980 ambazo zimeelezwa katika ujenzi wa vyumba vya madara pamoja na vyoo.
Chitukulo amesema kwamba fedha za Bost zilikuja maalumu kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu msingi ambapo zimeweza kujenga shule mpya mbili za msingi pamoja na vyumba vua madarasa katika shule mbali mbali za jiji la Arusha.
"katika utekelezaji wa mradi wa Boost ambao umetoa kiasi cha shilingi milioni 940.9.ambapo fedha zake zimejenga shule mpya ya Msasani na ujenzi wa madarasa 3 na vyoo katika shule ya muriet,vyumba 2 vya madarsa pamoja vyoo shule ya sinoni, Madarasa 5 na vyoo katika shule ya terati, darasa 1 na vyoo katika shule ya uhuru pamoja na madarasa 3 pamoja na vyoo katika shule ya Ukombozi". Amesema Chitukulo.
"Katika fedha za hazina ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 980 zimeweza kujenga shule mpya mbili ambayo ni shule ya Nafco na korongoni, Pia zimeweza kujenga vyumba 9 vya madarasa katika shule nne ambapo ni Arusha school vyumba 3, Naura vyumba 2, Meru vyumba 2 pamoja na unga ltd vyumba 2". Aliongeza Chitukulo.
Post A Comment: