Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
amewataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao kwa watoto katika malezi bora
ili kupunguza wimbi la watoto wa mtaani pamoja na kuzuia mmomonyoko wa maadili.
Ameyasema hayo jana usiku baada ya kufuturisha waumini
wa Dini ya Kiislam nyumbani kwake Ikulu ndogo Mkoani Shinyanga,ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa ni viongozi mbalimbali
wa serikali, viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM, viongozi wa Dini ya Kikristo,
wadau mbalimbali na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.
RC Mndeme amewaomba viongozi wa Dini kushirikiana
pamoja katika kutokomeza mmomonyoko wa maadili ambao husababisha watoto
kujiingiza kwenye uhalifu huku akisisitiza wazazi na walezi kuwalinda watoto wao
ili wakue katika maadili mema.
Amewaomba viongozi wa Dini kukemea suala la mmomonyoko
wa maadili linalopelekea baadhi ya vijana katika Mkoa wa Shinyanga kuiga mila na
desturi za kigeni ambapo RC Mndeme
ametumia nafasi hiyo kuwasihi vijana kufanya kazi halali kwa kuzingatia misingi
na taratibu wa Taifa hili la Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuomba Amani, umoja na mshikamano uendelee
katika Taifa hili ikiwa ni pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
na serikali ya awamu ya sita.
Amesema serikali ya Mkoa wa Shinyanga itaendelea kutoa
ushirikiano katika nyanja na sekta zote katika kutatua changamoto mbalimbali
ikiwemo changamoto za kiimani na zisizo za kiiamani huku akiomba ushirikiano
ili kuendeleza Amani ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Mndeme amewashukuru viongozi wa Dini kwa dua na
sala ambapo amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan inatambua na kuthamani kazi kubwa zinazofanywa na viongozi wa
Dini katika kuimarisha Amani Nchini.
“Viongozi wa dini mmekuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa letu katika Nyanja mbalimbali ikiwamo Sekta ya Afya na Elimu, sababu Taasisi zenu mmekuwa mkimiliki shule na huduma za afya pamoja na kudumisha amani, na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamani mchango wenu na itaendelea kushirikiana na ninyi siku zote,”amesema RC Mndeme.
Aidha RC Mndeme amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuwaombea watu watu huku akiisihi jamii kuwa na utamaduni wa majitoleo kwa watu wenye uhitaji wakiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi, wasioona pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kwamba hali hiyo itasaidia kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amemshukuru na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuguswa kufuturisha ambapo ametumia nafasi hiyo kumumbea dua pamoja na viongozi wengine akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Kitendo alichokifanya Mkuu Mkoa kwa kufuturisha waumini wa dini ya kiislamu ni kikubwa dhawabu yake atalipwa na Mwenyezi Mungu na atamzidishia zaidi ya alichotoa.Sisi viongozi wa dini tutaendelea kuliombea amani Taifa, pamoja na kumuombea na Afya njema Mheshimiwa Rais Samia na Serikali yake yote ili aendelee kuliongoza vyema Taifa na kuwaletea maendeleo Watanzania",
“Sisi tutaendelea kuomba Amani ya Taifa, pamoja na kumuombea Afya njema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia na Serikali yake yote kikiwamo na Chama cha Mapinduzi CCM, ili aendelee kuliongoza vyema Taifa na kuwaletea maendeleo watanzania”. amesema Sheikh Makusanya.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza
kwenye hafla ya futari Nyumbani kwake ikulu ndogo Shinyanga
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza
kwenye hafla ya Futari kwa waumini wa dini ya kiislamu iliyoandaliwa na Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme Nyumbani kwake ikulu ndogo Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi
akizungumza kwenye hafla ya Futari kwa waumini wa dini ya kiislamu
iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme Nyumbani kwake
ikulu ndogo Shinyanga.
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire awali akiongoza Swala ya saa 1 usiku nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire awali akiongoza Swala
ya saa 1 usiku nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya upande wa kulia awali akichukua
chakula kwa ajili ya kufuturu
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire upande
wa kulia awali akichukua chakula kwa ajili ya kufuturu
Zoezi la kuchukua chakula kwa ajili ya kufuturu likiendelea
nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ikulu ndogo Shinyanga
Zoezi la kuchukua chakula kwa ajili ya kufuturu likiendelea nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ikulu ndogo Shinyanga.
Zoezi la kuchukua chakula kwa ajili ya kufuturu likiendelea
nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ikulu ndogo Shinyanga
Zoezi la kuchukua chakula kwa ajili ya kufuturu likiendelea
nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ikulu ndogo Shinyanga
Post A Comment: