Na John
Walter-Manyara
Mkuu wa mkoa
wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi mkoani humo na maeneo
ya Jirani kuhudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya chanjo duniani yatakayofanyika
katika uwanja wa Kwaraa Mjini Babati siku ya Jumatatu April 24,2023 kuanzia asubuhi.
Taarifa ya
mkuu wa mkoa imesema tukio hilo litaambatana na shuguli mbalimbali zikiwemo
upimaji wa Afya na utoaji chanjo za magonjwa mbalimbali bure.
Kauli mbiu
ni "Tuwafikie wote kwa chanjo"
Mkuu wa mkkoa
amesema katika maadhimisho hayo, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya
Mhe. Ummy Mwalimu.
Amewataka
wananchi wote wahudhurie kwenye tukio hilo muhimu akisema "jamii iliyopata chanjo ni jamii yenye
afya"
Wiki ya
chanjo imetengwa maalum kwa ajili ya kuhimiza umuhimu wa chanjo kwa Watoto
wenye umri chini ya miaka 5 na wasichana wenye umri kuanzia miaka 14 ili
kuwakinga na maradhi mbalimbali hasa homa ya ini, surua na polio na wasichana
wenye umri kuanzia miaka 14 kwa ajili ya chanjo ya kinga ya saratani ya shingo
ya kizazi.
Post A Comment: