Kwa mujibu wa sheikh wa
Wilaya ya Shinyanga Soud Suleiman kategile amesema sikukuu ya eid el fitr
inategemea zaidi kuandama kwa mwezi,hivyo huenda ikawa kesho ijumaa au kesho kutwa
jumamosi
Sheikh kategile amesema
swala ya Eid itaswaliwa kiwilaya katika uwanja wa sabasaba kambarage Mjini
Shinyanga,ambapo ametoa wito kwa waamini wote wa dini ya kislaamu kushiriki ibada
hiyo muhimu.
Sheikh soud kategile
ameeleza kuwa Baraza la Eid el fitr litafanyika kwenye ukumbi wa Mikutano
uliopo CCM Mkoa wa shinyanga NSSF ya zamani,majira ya saa kumi jioni, na kwamba
mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya
waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu.
Sheikh huyo ametoa wito kwa waumini wa dini hiyo kutumia mafundisho waliyopata kwenye mwezi mtukufu wa ramadhani kuendelea na ibada pamoja na kuishi maisha yenye kumpendeza Mungu.
Post A Comment: